- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 11/10/2024
DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi akifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Hatujuani Ally Lukari, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na Watumishi wa Serikali na Wananchi kwa ujumla walifika mapema asubuhi leo hii na kujiandikisha katika Kituo cha Kujiandikisha wapiga kura cha S/Msingi Ngara Mjini.
Aidha, kabla ya kwenda kujiandikisha katika Kituo hicho Mhe DC Kahabi alipata nafasi ya kuongea na Waandishi wa habari wakiwemo Radio Kwizera, Bilomo online TV, na Juveila online TV na kutoa hamasa kwa Wananchi kuhusu zoezi la Uandikiahaji wapiga kura ambalo limeamza rasmi leo tarehe 11/10/2024 na litamalizika tarehe 20/10/2024.
Wananchi wa Wilaya ya Ngara wamekuwa na mwitiko na hamasa kubwa kutokana na maandalizi mazuri yanayoendelea kufanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg Solomon O. Kimilike (Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Ngara) na Afisa Uchaguzi wa Wilaya hiyo pamoja na wasimamizi wote wa zoezi la Uandikiahaji wapiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mhe Col Kahabi DC Ngara alijiandikisha kituo shule ya msingi Ngara Mjini.
Bi Hatujuani A Lukari Karibu tawala wilaya alijiandikisha Ngara mjini.
Kamanda wa TAKUKURU wilaya Ndg Ally Mikidadi Akijiandikisha katika kituo cha shule ya msingi Ngara mjini.
Afisa uchaguzi Ndg James Ling'hwa alikiwa na Msimamizi Msaidizi Halmashauri (hamasa) Ndg said Salum wakimpokea Mhe Col Mathias J Kahabi Mkuu wa wilaya.
Kamanda William Solla OCD Ngara Akijiandikisha.
Ndg Omary Rajabu Meneja TRA Ngara akijiandikisha.
Ngara Kazi inaendelea.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa