- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 05/02/2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika Ujenzi wa Jengo la Makao makuu Halmashauri unaoendelea Wilayani Ngara.
Mhe Kahabi akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg Solomon O Kimilike kwa pamoja wameridhishwa na Ujenzi huo ambao ulianza kwa kusua sua sana na ilipelekea Mkandarasi kutakiwa kujieleza na Kamati ya Usalama ya Wilaya inayongozwa na Mkuu Wa Wilaya Mhe Col Kahabi.
Aidha Mkandarasi aliweka commitment ya kuongeza kasi ya Ujenzi huo unaogharimu kiasi cha Shs bilioni 3.5 hadi kukamilika kwake.
Pamoja na kasi hiyo aliyonayo sasa Mkandarasi.
Mhe Mkuu wa Wilaya Mhe Kahabi amesema anataka kuona mafundi hao wanajenga usiku na mchana ili kukamilisha Ujenzi huo ndani ya muda.
Aidha mradi huo kwa hivi sasa umefikia asilimia 43.8 na kulingana na Mkataba unatakiwa kukamilika tarehe 31/03/2024.
Kazi iendelee.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa