- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara leo tarehe 02/8/2024 ameshiriki kuwapokea Waandesha Baiskeli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakitokea Nchi jirani ya Burundi.
Mapokezi hayo yamefanyika katika Mpaka wa Tanzania na Burundi, eneo la Kabanga OSBP. Waendesha baiskeli hao walifika katika eneo la mpaka huo wakiongozwa na Mhe Balozi Remy Barampama ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Vijana, Utamaduni na Michezo Nchini Burundi.
Waendesha baiskeli toka Nchi wanachama wa EAC watazunguka Nchi za EAC ikiwemo, DR Congo, Burundi, Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda na watatumia muda wa siku 56 kumaliza tour hii iliyopewa jina la GACS - Great Africa Cycling Safari.
Kiongozi na mwanzilishi wa tour hii raia wa Uganda Ndg Johnbosco Palongo amesema lengo la tour hii ni kuongeza ufahamu kuhusu EAC integration, kutoa Elimu kuhusu Mabadiliko ya tabia ya nchi/athari zake na Usalama wa chakula miongoni mwa Nchi wanachama wa EAC.
Mhe DC Kahabi, amewakaribisha sana Waendesha baiskeli hao Nchini Tanzania kupitia Wilaya ya Ngara katika Mkoa wa Kagera na kuwahakikishia Amani na Usalama muda wote watakapokuwa Wilayani Ngara. Aidha limefanyika zoezi la upandaji miti na kuongea na wananchi ng'ara mjini ili kufikisha ujumbe
Mhe Col Kahabi Amewapongeza Viongozi wote akiwemo Kiongozi wa Waendesha baiskeli pamoja na Viongozi wawakilishi wa Serikali ya Burundi waliofuatana na vijana hao.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa