- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkandarasi Asimamishwa Kazi na Kutakiwa aeleze Changamoto za Kuchelewa Mradi Kukamilika.
Tarehe 09/02/2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara akifuatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Enock Ntakisigaye, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mhe Diwani na Mtendaji wa Kata ya Kanazi, Viongozi wa LADP pamoja na Uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Remela walifanya Ukaguzi wa uwanja wa Michezo Remela ambao unaendelea kufanyiwa Maboresho kwa kupanda nyasi pamoja na maboresho mengine kuzunguka uwanja huo.
Baada ya ukaguzi huo imebainika kuwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo ameweka msimamizi ambaye hata BOQ hana na hajui lolote.
Aidha, msimamizi huyo baada ya kubainika kasoro nyingi katika Utekelezaji wa mradi.
Mhe Mkuu wa Wilaya Col Kahabi amemwagiza asimame kuendelea na usimamizi hadi Mkandarasi anayeishi Mwanza atakapofika Wilayani Ngara tarehe 12/02/2024 kwa ajili ya kujibu hoja na changamoto mbalimbali zilizobainika katika mradi huo.
Mradi huo wa upandaji Nyasi unatekelezwa kwa gharama ya Tsh Milioni 23 kulingana na Mkataba.
Mhe Mkuu wa Wilaya Col Mathias J Kahabi akiwa na timu aliyoambatana nayo wakikagua uwanja wa michezo Uliopo Remela kata ya kanazi wilayani Ngara.
Mhe Mkuu wa Wilaya akiwa na viongozi aliyefuatana nao kukagua uwanja wa michezo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa