- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Leo tarehe 01 Novemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe Col Mathias Kahabi amesaini Majendwali ya riba za fidia kwa waguswa wote wa Mradi wa Tembo Nickel.
Mara baada ya kusaini Majedwali hayo, Mhe DC Kahabi ameupongeza Uongozi wa Tembo Nickel uliowakilishwa na ndg Moses Rusasa - Afisa Mahusiano wa Mradi huo kwa kitendo cha kulipa riba na kuhakikisha kila Mwananchi anapata haki yake yote anayostahili kupata bila urasimu wala ucheleweshaji wa aina yoyote ile.
Mhe Kahabi Dc Ngara amesema kitendo hicho cha kuheshimu sheria za Nchi na Kanuni za Kimataifa cha kulipa riba hiyo kwa wakati, ni Kitendo cha Uaminifu na kinaleta imani kubwa kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, malipo haya yamesaidia kuondoa manung’uniko na malalamiko kwa baadhi ya Waguswa ambao walihisi malipo haya yangechelewa kulipwa ndani ya muda ulioahidiwa na Mradi wa Tembo Nickel .
Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya Ngara akisaini.
Viongozi wa Tembo Nickel wakimwonesha orodha mhe Col Kahabi Mkuu wa wilaya.
Ngara Kazi inaendelea.............
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa