- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 08/10/2024, DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi ameendelea na ziara yake ya usimamizi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ngara iliyopo Kata ya Mbuba Tarafa ya Rulenge ambapo shughuli mbalimbali za Ujenzi zinaendelea katika Hospitali hiyo ya Wilaya.
Mhe DC Kahabi anawapongeza timu ya Wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndg Solomon Kimilike kwa kuweka mikakati ya pamoja mahsusi kwa ajili ya kumalizia Ujenzi huo ambapo huduma muhimu katika Hospitali hiyo zilianza kutolewa toka tarehe 01/5/2024.
Aidha, kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias Kahabi kipekee kabisa anampongeza sana Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia Halmashauri yetu kiasi cha Tshs bilioni 1.8 ambazo zinafanikisha kujenga Hospitali ya Wilaya ya Ngara.
Ngara Kazi inaendelea.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa