- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi, tarehe 23/08/2024, akifuatana na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Usala ,Wilaya walifika eneo la Kabanga OSBP kwa ajili ya kutatua Mgogoro uliokuwepo kati ya vijana waliokuwa wanafanya kazi ya kulipa ushuru wa Road Toll kwa niaba ya madereva wa magari makubwa ya mizigo toka Burundi kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Kabanga.
Akitoa taarifa kwa DC Ngara kuhusu vijana hao na Mgogoro uliokuwepo Border Manager wa Kabanga OSBP Ndg Laurent Kagwebe alisema vijana hao toka pande zote mbili (Burundi na Tanzania) walikuwa wanafanya kazi ya kulipia ushuru wa Road Toll kama agents wa madereva wa magari makubwa ya mizigo toka Burundi kwa makubaliano yao(ujira) na madereva wa magari hayo.
Border Manager alifafanua kuwa kazi hiyo ilikuwa inafanyika kinyume na sheria za Forodha - TRA. Kutokana na changamoto hiyo pale vijana walivyoelezwa kuwa wanafanya kazi kinyume na sheria waliona kama wanadhulumiwa haki ya kupata riziki yao halali, ndipo waliomba kukutana na Mkuu wa Wilaya NGARA kwa maelekezo zaidi.
DC Ngara Mhe Col Mathias Kahabi baada ya kuwasikiliza vijana hao kwa kina ametoa maagizo ya kusimama kwa shughuli za vijana kulipia ushuru wa Road Toll mpaka pale utaratibu mwingine ulio bora zaidi utakapoandaliwa ambao hautakinzana na sheria za Forodha zilizopo katika kutekeleza majukumu yake. Aidha, walipokea vema maelekezo hayo ya Mkuu wa Wilaya na kuahidi kuwa watulivu wakati suala lao linaendelea kufanyiwa kazi.
Ngara Kazi inaendelea...........
ngaradc. go. tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa