- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanajamii wa shule ya sekondari ya Lukole katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kudumisha nidhamu, ili waendelee kushika nafasi ya kwanza katika shule za sekondari mkoani Kagera, kwenye mthani wa kidato cha sita mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wiulaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, ameyasema hayo Machi 29, 2019 wakati akikabidhi cheti cha pongezi kwa uongozi wa shule hiyo wakati wa Mahafali ya sita, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti.
“Tulikusanya vyeti vinne, ambapo shule zangu zote zilifanya vizuri, lakini Lukole sekondari ikiwa ya kwanza; tafsiri yake ni kwamba shule ya Lukole ina nidhamu, kwa sababu mahali penye nidhamu, ushirikiano na umoja ndipo matunda mazuri yanatoka.” Alisema Ndugu Bahama.
Kwa hiyo, ufaulu huu ni matokea ya uwepo wa nidhamu shuleni, nishamu ya walimu, nidhamu ya wanafunzi na nidhamu ya wafanyakazi wasio walimu, kwa sababu mtoto ambaye hana nidhamu hana nafasi kwenye shule zetu.
Amesema vijana 342 wasichana 116 na wavulana 226 wameweza kuhitimu masomo yao, kwa sababu ya kuwa na nidhamu, huku akidai kuwa shule ya sekondari Lukole ni sehemu sahihi ya wanafunzi kujifunza kulingana na jiografia, na umahili wa walimu wao.
“Hatutegemei kwamba sifa ya ufaulu tuliyonayo, ambapo kwa kipindi cha miaka sita tumefaulisha kwa 100%, kwamba mwaka huu itapungua; ni matumaini yangu kwamba wanafunzi hawa watafaulu kwa 100%, lakini kwa kuanzia daraja la I na II.” Alisema Bahama.
hata hivyo, amewapongeza wazazi kwa malezi yao yaliyotukuka ya kitanzania na hatimaye kuwawezesha kuifikia siku ya leo, ambapo watoto wao wanahitimu masomo yao; huku akidai kwamba, mzazi mwenye nidhamu uzaa na kulea watoto wenye nidhamu.
Risala ya wanafunzi pamoja na mambo mengine waliomba wapewe kompyuta ili ziwasaidie katika kujifunza, Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kuwaongezea kopmpyuta pindi atakapowiwa, maana Tumaini Fund walikuwa wamewapatia kompyuta tayari.
“Hata siku moja mtu binafsi hawezi kumiliki ardhi ya shule” hilo ni tamko la Waziri wa Ardhi, na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi alilotamka alipokuwa Wilayani Ngara mwaka 2018, Ndugu Bahama alikariri tamko hilo, kuonyesha makosa ya baadhi ya wananchi, wanaojitwalia ardhi za shule kwa nguvu.
Amesema hawezi kumpa haki mtu mmoja na kuwaacha 600, wakiwa hawana mahali pa kujenga miundombinu ya shule, huku akiahidi kuwatuma maafisa ardhi, wafanye tathimini na ikigundulika mwananchi huyo ana haki ya kumiliki ardhi hiyo, atampatia ardhi nyingine.
“Niwaombe mvute subira wakati tukiangalia jinsi ya kutatua changamoto hizi; kwa mfano, hapa naona upungufu wa nyumba za watumishi, mimi pamoja na watendaji wenzangu katika Halmashauri tutajipanga tuweze kufanya mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.” alisema Ndugu Bahama.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kutoa ushirikaino wa kuziwezesha shule hizo pindi watakapotakiwa kufanya hivyo kwa madai kwamba shule za sekondari hususani hizi za kidato cha tano na cha sita, zinamilikiwa na wazazi na Halamshauri kama serikali.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa