- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wameshauriwa kutumia mifumo ya kibeki iliyoenea nchini, ili waweze kuepuka matatizo mbalimbali yakiwemo ya fedha bandia na kuvamiwa.
Hayo yamesemwa na Meneja Msaidizi Kitengo cha Sarafu Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza ndugu Ilulu said Ilulu, wakati akitoa semina ya jinsi ya kuepuka fedha bandia Aprili 27, 2018, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Amesema biashara ya noti bandia katika nchi ya Tanzania imepungua kwa kasi, kwa sababu wananchi wanatambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya kifedha, iliyopo hapa nchini.
“Tunawashauri wananchi wote, kwamba wanapopata tatizo la kubambikiziwa noti bandia; ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, watoe taarifa mara moja katika vyombo vinavyohusika, ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.” Alisema ndugu Ilulu.
Meneja huyo amewataka wananchi kutunza noti ili zisichakae, kwani zikidumu kwa muda mrefu, zinasaidia kupunguza gharama za kurudufu noti mpya; fedha ambayo ingetumika kutengeneza noti mpya inatumiaka katika shughuli za maendeleo.
Aidha, ameonya kwamba watu waepuke tabia ya kulipwa fedha kwa keshi, kwani ni hatari, ambazo amezitaja kuwa ni ama kuvamiwa au kupata noti bandia. Semina hiyo imedumu kwa siku moja na imewahusisha wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa