- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wafanyabisahara katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kufanya biashara kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali, ili waweze kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza kwa kuvusha bidhaa kwa kutumia njia za panya.
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka ya Biashara na Masoko ndugu Christopher Chiza, ameyasema hayo wakati akiongea na wafanayabiashara wa Ngara mjini, na Kabanga Aprili 13, 2018, katika ukumbi wa Halmashauri na Kabanga sokoni.
Amesema kukwepa kodi kunalisabiashia taifa kukosa kodi; huku akisistiza kuwa si hilo tu kwani madhara yake yanawafuata hata wafanyabiashara hao, kwa kupata madhara na hasara pia.
Aidha, amesema kuwa lengo la ziara yao nikuwafahamisha wadau shughuli za udhibiti wa biashara, zinazofanywa na Mamlaka ya biashara na masoko, pamoja na kuwatangazia fursa zinazopatikana katika nchi zinazotuzunguka.
“Wafanyabiashara wetu lazima wazijue fursa na changamoto zilizoko katika nchi jirani, na Mamlaka ya biashara na masoko inao wajibu huo, na lengo hasa la kikao chetu ni hilo.” Alisema ndugu Chiza.
Kwa upande wao, wafanyabiashara walishukuru uongozi wa Mamlaka kwa kuwapanua mawazo, kwani wamejifunza vitu vingi kinyume na matarajio yao, wameomba kupata mafunzo, ili yaweze kuwapatia mwanga zaidi; wazo aliloridhia Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo.
Hata hivyo, wamesema wanakero nyingi zinazowakabili likiwemo la kukatika kwa umeme, kodi kubwa pamoja na vikwazo wanavyopata, wanapokwenda kuuza bidhaa nchi jirani; Mwenyekiti huyo wa Mamlaka amewaahidi wadau hao kuwa atayafanyiakazi matatizo yao.
Kikao hicho kiliwajumuisha wafanyabiashara wa mjini Ngara, Rulenge, Rusomo na Rulenge pamoja na wale wa Kabanga, na wajumbe walipata fursa ya kuongea na uongozi wa Mamlaka ya Mapato mpakani Kabanga.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa