- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Hizi fedha si zawadi bali ni mkopo, na kwasababu ni mkopo lazima zirejeshwe, ili tuweze kuvikopesha vikundi vingine vinavyohitaji kama nyinyi.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama.
Ndugu Bahama alisema hayo wakati akitoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya milioni 16, kwa vikundi 08 vya wakina mama na vijana kwenye ukumbi wa Halmashauri Julai 04, 2018; kwamba fedha waliyopkea inatakiwa izunguke kutoka kikundi kimoja kwenda kingine.
Amesema nidhamu ya fedha waliyoonyesha mwanzo hadi wakachaguliwa kati ya vikundi vingi katika Halmashauri ya Ngara, wanatakiwa kuionyesha katika fedha waliyopewa Julai 04, 2018.
Ameonya kwamba yeye ndiye msajili wa vikundi vya akina mama na vijana, ikiwa kikundi akitokuwa na nidhamu ya fedha atakifungia mara moja, kwani hatakubali fedha ya serikali ipotee wakati amepewa dhamana ya kuilinda fedha hiyo.
“Ninazo taarifa ambazo sijazithibitisha bado, kwamba tukiwapa fedha mnazingawana; yaani kila mmoja anapata fedha yake badala ya kutumia fedha hiyo kama kikundi, kama vikundi ni vya namna hii bora hiyo fedha tusiwape.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bahama.
Serikali inasisitiza vikundi vilivyopewa mikopo kurejesha fedha hiyo, kwa wakati kwa sababu fedha iliyokopeshwa inaporejeshwa vinakopeshwa vikundi vinangine; na kwa mtindo huo tutawasaidia watu wengi kujikwamua kiuchumi, ambalo ndilo lengo la serikali.
Naye mmoja wa wanufaika wa mkopo huo Mdugu Imelda Bideberi, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwaamini na kuona kazi wanazozifanya kuwa zinawapa ridhaa ya kupata mkopo, na kwamba watatumia mikopo hiyo kwa lengo lililokusudiwa.
Aidha, ameahidi kwamba watarejesha mikopo hiyo kwa wakati, ili iweze kuwanufaisha wengine wanaohitaji, ili kutimiza azima ya mikopo hiyo kwa vijana na akina mama.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa