- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro anawajulisha Wananchi wa Jimbo la Ngara kuwa ahadi yake ya kuhakikisha Wananchi wa Ngara wanapata huduma ya Maji safi inaendelea kutekelezeka.
Mnamo tarehe 22/10/2023 mitambo ya kuchimba visima virefu vya maji imefika katika Kijiji cha Mkalinzi ili kuwachimbia wananchi na wakazi wa hapo kisima cha maji.
Vile vile Mkandarasi anayejenga Mradi wa maji wa Kabanga yupo anafunga pump ya maji kwaajili ya kufanya majaribio ya kusukuma maji. Mradi huu unatarajia kumaliza kero ya Maji kwa Wananchi wa Kabanga pamoja na maeneo ya Kumuzuza, Kata ya Mabawe.
Upande wa Kasange, Kanyinya, Kumubuga, Rusumo, Kihinga nako kuna wakandarasi ambao wapo kwenye hatua za mwishoni za kukamilisha Miradi ya Maji na baadhi ya maeneo Miradi imekwishaanza kufanya kazi.
Bugarama Mradi umekamilika sambamba na Kanazi na Kabalenzi. Vile vile Uchimbaji wa kisima kirefu Murusagamba umekamilika kwa asilimia mia moja na kazi iliyobakia ni kujenga kisima hicho na kukiunganisha kwenye njia ya kusambaza Maji safi kwa Wananchi.
Kwa upande wa Katerere, Mhe. Mbunge ametoa fedha yake Binafsi ili kununua pump, nyaya, Tank na Bomba za kusambaza maji ya kisima cha Kitongoji cha Katerere wakati ambapo Serikali inaendelea na mchakato wa kumpata mkandarasi wa kujenga mradi mkubwa wa Maji wa Katerere.
Hivi karibuni NGUWASA ilisaini mkataba na Kampuni ya Kuchimba Visima vikubwa viwili ili kuongeza uzalishaji wa Majisafi Ngara mjini kama ambavyo Mhe. Mbunge aliahidi kwenye mikutano mbali mbali.
Mhe. Mbunge anaendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza Miradi mbalimbali kwa Wananchi. Vile vile anawashukuru Watendaji Wakuu wa Serikali Wilayani Ngara pamoja ma Madiwani ambao wanafanya kazi kubwa ya kuwasemea wananchi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa