- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Gari lenye usajili wa namba T494AKC, likitokea kata za Nyakisasa na Rulenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, limekamatawa likisafirisha magunia 389 ya mahindi, likiyapeleka mkoani Singida bila kulipia ushuru.
Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Ndugu Ghalib Mkumbwa, amesema gari hilo limekamatwa Machi 26, 2018, katika kizuizi cha Kumubuga kata ya Murusagamba.
“Dereva wa gari hilo anaitwa ndugu Emanuel Kingu mkazi wa Kahama, alitudanganya kwamba ana maguania 200 tu ya mahindi, tulipofanya upekuzi tulikuta ana magunia 389, tukampiga faini ya shilingi 1,067,000.” Alisema Ndugu Mkumbwa.
Amefafanua kwamba kila gunia amelipia Shilingi 3000/=, ambayo jumla yake ni shilingi 567, 000/=, na akalipia faini ya shilingi 500,000/= ya udanganyifu.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Erick Nkilamachumu, amewataka wafanya biashara kulipa mapato ya serikali, ili waepuke usumbufu wa kupelekwa mahakamani.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa