- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakurugenzi wa Halmashauri zote hapa nchini wametakiwa kutoa ushikiano kwa wakuu wao wa idara ili wahakikisha mfumo wa kutambua viashiria hatarishi unaanzishwa na unatumika ili kuzisaidia Halmashauri hizo kufikia malengo waliyojiwekea.
Wito huo umetolewa na Mkaguzi wa Ndani Ofisi ya Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wizara ya Fedha Ndugu Onesimo Mbekenga Julai 24, wakati wa mafunzo kazini yaliyowajumuisha wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Ndugu Mbekenga amesema kwamba serikali iliamua kuanzisha mfumo huu wa usimamizi wa vihatarishi kwenye Halmashauri na taasisi za umma ili ziweze kufikia malengo yake waliyojiwekea.
“Mfumo huu unasaidia kudhibiti vihatarishi ambavyo havikutarajiwa wakati taasisi zinaweka malengo yake, na kwamba vihatarishi hivyo vinaweza kuwa vizuizi vya kuwazuia msifikie malengo yenu kabisa au kwa wakati mliopanga.” Alisema Ndugu Mbekenga.
Kwa wakuu wa idara wanawajibu kuainisha vihatarishi kulingana na malengo waliyojiwekea katika idara zao; hivyo mfumo huu utawasaidia kutambua matatizo yalipo, badala ya kusubiri hadi mwishoni na kuanza kushika uchawi.
Kwa hiyo, kuwa na huu mfumo kunaisaidia Halmashauri kutambua vihatarishi ambavyo havikutarajiwa kuweza kujitokezaa na kusababisha madhara kwenye mipango na malengo waliojiwekea.
Kuanzisha mfumo huu serikali inalenga kupunguza viashiria hatarishi katika Halmashauri na taasisi zake ili ziweze kufikia malengo yaliyopangwa na serikali kufikiwa katika kutekeleza miradi husika.
Mfumo huu unawahakkikishia wadau wa taasisi za umma kwamba malengo yaliyopangwa yataweza kufikiwa au la; huku ukirahisisha mawasiliano kati ya mkuu wa idara na wakuu wengine wa idara pamoja na watumishi ndani ya Halmashauri husika.
Ameonya kwamba kutozingatia mfumo wa kuthibiti vihatarishi kazini kunaweza kusababisha kutofikia kwa malengo ya Halmashauri; hivyo akawataka wakuu hao wa idara kutumia mfumo huu.
Wakuu wa idara wameishukuru Ofisi ya Ukaguzi wa Ndani Wizara ya Fedha, kwa kutambua mapungufu yaliyokuwa yakijitokeza katika Halmashauri na Taasisi za serikali, katika kukabiliana na viashiria hatarishi.
Aidha, wamesisitiza kwamba zoezi hili liwe endelevu, ili Halmashauri na taasisi za umma ziweze kufikia malengo na kuyafikia; huku wakizibi viashiria ambavyo vinaweza kuwa vikwazo katika kufikia malengo yao.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa