- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watendaji wa kata na vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kusimamia misingi, na maadili ya uongozi wao, wakati wanafuatilia watoto waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, ambao hawajaripoti shuleni mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele ameyasema hayo Machi 02, 2018 wakati akifunga kikao cha kamati ya ushauri cha wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
“Kuna tetesi kuwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji mnachukua fedha kwa wazazi ili wasiwapeleke watoto shuleni, tabia hiyo ikome mara mara moja; mnatakiwa kuzingatia misingi ya uongozi na maadili ya kazi yenu; kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yenu.” Alisema Lt. Col. Mntenjele.
Amesema wakati tunaelekea mwishoni mwa watoto hao kuripoti shuleni, ambayo ni Machi 30, 2018, watendaji wote wanatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji ya wanafunzi, ambao hawajaripoti shuleni ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wazazi wanaozorotesha zoezi hili.
Aidha, wajumbe wa kikao hicho walishauri kuwa katika shule zenye walimu wawili au zaidi wanaofundisha masomo ya aina moja, wahamishiwe katika shule ambazo zina uhaba wa masomo hayo ili kuleta ufanisi Zaidi.
Walimtaka Afisa elimu sekondari kuhakikisha kuwa walimu wa masomo ya sayansi wanapelekwa kwa kila shule, ili wanafunzi waweze kufundishwa masomo hayo ipasavyo.
Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Afisaelimu sekondari ndugu Jared Nyaonge amesema kuwa kwa sasa walimu wanapangiwa vituo vya kazi kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), hivyo wanaripoti moja kwa moja vituoni kwao (shule walizopangiwa); kwa hiyo ofisi ya elimu sekondari haina mamlaka ya kuwabadilishia vituo walivyopangiwa.
Idara ya Elimu sekondari wiilayani inaendelea kubaini upungufu wa walimu wa sayansi, na kuwasilisha mapendekezo ya mahitaji kwenye ngazi ya Mkoa kwa utekelezaji zaidi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa