- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Niwatoe wasiwasi watanzania wote kwamba hakuna mtu, ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa wa ebola ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.” alithibitisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Umi Mwalimu wakati alipofanyaziara katika mpaka wa Tanzania na Rwanda Rusumo.
Amesema kwamba kila mgonjwa anayeigia nchini Tanzania, lazima apimwe afya yake kwani mgonjwa wa ebola akiruhusiwa kuingia nchini; Tanzania itakuwa katika hatari ya kupata maambukizi hatari ya ebola.
“Nimefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Rwanda, Rusumo, ili kuangalia utayari wa mkoa wa Kagera katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, kama nilivyotoa taarifa wiki iliyopita, kwamba mlipuko wa ugonjwa wa ebola nchini Kongo unaiweka Tanzania katika hatari ya kupata wagonjwa huo.” alisema Mh. Mwalimu.
Alielekeza kwamba wakati wasafiri wanaopita katika mipaka rasmi wanadhibitiwa, lazima kuwepo makusudi ya kudhibiti changamoto ya wasafiri wanaopita njia za panya hasa, ambao wanatokea nchini Burundi.
Iliamuliwa kwamba kila wilaya ya mkoa wa Kagera hasa mpakani mwa Burundi, wahakikishe kunakuwa na zahanati iliyotengwa mahsusi, kwa ajili ya kuwapokea wagonjwa watakathibitika na kuhisiwa kuwa na ugonjwa wa ebola.
Wagonjwa watakaohitaji huduma zaidi katika mkoa wa Kagera, watapelekwa katika wilaya ya Karagwe kwa ajili ya matibabu zaidi, na kwamba si wagonjwa wote watapelekwa kutibiwa Karagwe.
Aidha, amesema kwamba kuwepo kwa ugonjwa wa ebola nchini, kunaweza kukwamisha mambo mengi aliyoyataja kuwa ni kusimama kwa biashara, kufutwa kwa safari za ndege na hata kudorola kwa uchumi wa nchi.
“Tumeteua maabara za Bugando, KCMC na hospitali ya taifa ya Muhimbili zitumike katika kupima watu wanohisiwa na kuthtibitika kuwa na ugonjwa wa ebola, na kwamba sampuli za wagonjwa zitachukuliwa na kufanyiwa uchunguzi katika maabara hizo.” alisema Mh. Mwalimu.
Wananchi wa vijiji vinavyopokea watu kutoka nchi jirani wahakikishe, wanafuata taratibu za uhamiaji; huku akisisitiza kwamba mtu akishaingia nchini akathibitika kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola apewe huduma ya afya mara moja.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa