- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Idara ya Elimu msingi na sekondari mkoani Kagera, imeazimia kufaulisha kwa asilimi 95 kwa wanafunzi, watakaofanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na saba, pia kufuta daraja la nne na sifuri kwa wanafunzi, watakaohitimu kidato cha nne mkoani humo.
Azimio hilo limewekwa wazi Januari 28 ,2019 na Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera Ndugu Aloyse Kamamba, alipokutana na walimu wa vitengo mbalimbali na maafisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Ngara, akiwa katika ziara ya kuhamasisha uboreshaji wa taaluma.
Ndugu Kamamba amesema; walimu wanatakiwa kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi na vifaa kwa kila somo, wakilenga kufaulisha wanafunzi, huku wakihakikisha hakuna wanafunzi wanaobaki nyuma kitaaluma, na kuwasaidia wazito kuelewa.
“Naomba niwe wazi kwa hili, mwalimu atakayeshindwa kutekeleza malengo tuliyojiwekea kimkoa, hana budi kutafuta kazi nyingine kabla ya hatujamuondoa, kwani atakuwa hakusanyi pamoja nasi, bali anatawanya” Alisema Kamamba
Amesema serikali imewekeza katika sekta ya elimu, ambapo indara ya elimu mkoa wa Kagera inapokea zaidi ya Shilingi bilioni 1.5; hivyo hakuna kiongozi, atakayemvumilia mwlimu mzembe, katika utekelezaji wa mikakati ya kufaulisha wanafunzi.
Katika hatua nyingine, amewapongeza walimu kwa juhudi wanazofanya katika utendaji kazi; licha ya chanhgamoto mbalimbali wanazokabiriana nazo kama vile kufanyakazi katika mazingira magumu.
“Kwa ujumla mkoa wetu umefanya vizuri kwa kushika nafasi ya nane kati ya mikoa 31, na mwaka juzi tulikuwa nafasi ya tisa, kwa hiyo, tumepanda nafasi moja, nafasi moja hii si haba, kwa sababu mikoa yote inajitahidi kufanya vizuri.” Alisema Ndugu Kamamba.
Kuna baadhi ya Halmashauri, ambazo hazikutimiza wajibu wao, kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Muleba, Bukoba Vijiijini, na Kurwa, amesema uwajibikaji wa halmashauri hizo ulikuwa hafifu, huku akidai kwamba wamefanya vikao kazi na Halmashauri hizo kuona kwamba mwaka 2019 wanafanya vizuri zaidi.
Katika vikao kazi hivyo amesema kwamba kwa wasiotimiza wajibu wao hatua inayofuata ni kuwawajibisha kisheria na kwamba kila mmoja azibe pengo alilolitengeneza mwaka 2018, ili mkoa uweze kufanya vizuri mwaka 2019.
Kupanda na kushuka kwa Mkoa wa Kagera katika mitihani ya Taifa, kunatokana na uwajibikaji hafifu wa viongozi ngazi za wilaya, lakini maafisaelimu kata nao hawatimizi wajibu wao ipasavyo pamoja na kupewa vitendeakazi, pia walimu wakuu wasipotimiza wajibu wao, matokeo yanayopanda na kushuka.
“Kielimu tuko vizuri kimkoa, mwaka 2018; mtihani wa darasa la nne mkoa wetu, umeshika nafasi ya kwanza, lakini mithani wa dararsa la saba umeshika nafasi ya tano; kidato cha pili mkoa umeshika nafasi ya saba, laikini kidato cha nne umeshika nafasi ya nane.” Alisema Ndugu Kamamba.
Mwaka 2018 Mkoa huo ulipanga kuwa na ufaulu wa asilimia 88 ambapo wanafunzi 25,499 wamejiunga na kidato cha kwanza 2019 katika awamu ya kwanza kwa kuzingatia vyumba vya madarasa vilivyopo, kati yao wavulana ni 14,356 na wasichana 13,143 sawa na asilimia 64.4 .
Vile vile Afisa Taaluma wa mkoa wa Kagera Ndugu Fidelis Apolinary, amewataka walimu kufuata taratibu na miogozo iliyowekwa na serikali, kuhakikisha watoto wanafaulu; badala ya kusingizia changamoto zilizomo katika sekta ya elimu.
“Visingizio vya kutopandishwa madaraja na mishahara, havina maana, kwani hapa Tanzania hakuna mkoa wowote walimu, walipopandishwa madaja wala kuongezewa mishahara, lakini mkoa wa Kagera, tumekuwa wa nane wakati kuna mkoa umekuwa wa kwanza, tuwajibike.” Alisema Apolinary.
Pia, katika kikao hicho walimu wa mkoa huo, kwa kushirikiana na wazazi, wameagizwa kuanzia Marchi 31 mwaka huu, wanafunzi wapate chakjula au uji shuleni, na utekelezaji wake usimamiwe na wananchi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa