- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imepata hati safi ya taarifa ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018. Akisoma ripoti ya majibu ya hoja za CAG, Muhasibu wa Halmashauri ya Ngara Ndugu Yona Charugamba alieleza kuwa Halmashauri ya Ngara iliweza kujibu hoja za CAG kwa uhakika na ufasaha ikiwa pamoja na kuwasilisha nyaraka na vielelezo 100 vilivyohitajika tofauti na 43 kama ilivyokuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Saada Malunde aliyekuwepo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkuu wa Wilaya ya Ngara,Mwenyekiti Halmashauri Ngara Mhe. Eric Nkilamachumu,Mkurugenzi Mtendaji Ngara Ndugu Aidan Bahama,Mbune wa Ngara Mjini Mhe. Alex Gashaza,Baraza la Madiwani pamoja na wakuu wa vitengo/idara wa Halmashauri ya Ngara.
Mgeni rasmi wa kikao hicho Mhe. Saada aliipongeza menejimenti ya Halmashauri ya Ngara ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Aidan J. Bahama kwa kazi nzuri wanayofanya . Pia aliiomba Halmashauri kumtumia vema Mkaguzi Mkuu wa Ndani ili kuzuia kuibuka kwa baadhi ya hoja ambazo zinaweza kumalizwa na Halmashauri yenyewe.
Baraza la madiwani liliiridhia na kuipitisha taarifa iliyosomwa na Mweka hazina wa halamshauri ya Ngara.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa