- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imeamua kulifufua na kulirejesha zao la kahawa chini ya Chama cha Ushirika, ili kuinua uchumi wa wakulima uliokuwa ukididimia baada ya kuuza huria kahawa yao kwa wafanyabiashara.
Akiwasilisha mfumo mpya wa uendeshaji wa zao la kahawa katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Machi 02, 2018, Afisa Kilimo wa wilaya ya Ngara Ndugu Constantine Mudende, amesema kuwa Halmashauri imeamua kurudisha zao la kahawa kwa wakulima wenyewe.
“Tutawasadiia wakulima wetu tangu kuandaa vitaru vya miche ya kahawa hadi kuwatafutia masoko ili waone faida ya jasho lao, huku tukiwasaidia kujikwamua kiuchumi.” alisema ndugu Mudende.
Amesisitiza kuwa ili kufanikisha azima hiyo wakulima wa kila kijiji wilayani Ngara, wanatakiwa kujiandikisha ili wajulikane, na kuwaomba maafisa watendaji wa vijiji na kata kufanikisha zoezi hilo.
Ameonya kuwa kahawa yote itakayovunwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, itauzwa kwenye chama cha ushirika na si vinginevyo, na kuwataka wafanyabiashara kununua kahawa hiyo mnadani na si kwa wakulima moja kwa moja.
Ndugu Mudende ameiomba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kudhibiti kahawa itakayopatikana ili isiuzwe kimagendo, nakuwataka kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka agizo hili, ili iwe fundisho kwa wengine.
Amependekeza kuwepo na vyama vya msingi kila ngazi za vijiji, na kuongeza kwamba ofisi ya Kilimo ya wilaya ijiwekee utaratibu wa kukutana na wadau wa zao hili angalau mara mbili kwa mwaka.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa