- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maedeleo inaendelea kutoa na kuboresha huduma za lishe kwa jamii hasa siku 1000 za uhai wa mtoto tangu mimba kutungwa ili kuondoa tatizo la hali mbaya ya lishe.
Akiongea katika kikao cha robo ya nne Afisa Lishe Ndugu Seleman Hamis alisema katika kipindi cha April –Juni cha mwaka wa fedha 2018/2019 shughuli zilizofanyika ni kampeni ya utoaji wa matone ya vitamin A na dawa za minyoo ambayo ilifanikiwa kwa asilimia 91% katika utoaji wa Vitamini A na asilimia 94% kwa dawa za minyoo.
Shughuli nyingine ni upimaji wa utapiamlo mkali kwa kutumia utepe wa kupimia mzingo wa mkono (MUAC Tape).Pia Usimamizi shiriki katika vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii ulifanyika.
Afisa Afya aliongeza kuwa tathmini na ufuatiliaji wa kaya zenye watoto waliokuwa katika darasa la utayarishaji vyakula baada ya miezi 3 (siku 90) ilifanyika pamoja na kufanya vikao vya mwezi kwa wasimamizi wa Afya jamii (WAJA).
Licha ya juhudi hizi zilizofanywa na Sekta ya lishe ikishirikiana na taasisi za kimaendeleo,kuna changamoto ambazo bado zinapelekea zoezi la kuhakikisha kila kaya inapata lishe bora kupunguzwa kasi.Changamoto kama watoto wengi kutokupimwa utapiamlo kipindi cha kampeni,kutokujaza taarifa katika kolamu ya 18 MTUHA,ukosefu wa kitabu cha Afya ya motto na mbao za kupimia urefu kwa ajili ya ufuatiliaji wa maendeleo na ukuaji wa mtoto, Upungufu wa idadi ya WAJA wenye mafunzo,umbali wa vijiji,ulevi uliokithiri wa wazazi na kata kutokuwa na chakula cha kutosha.
Mwenyekiti wa kikao Ndugu Gideon Mwesiga alishauri kufanyike juhudi ili kupunguza changamoto ikiwa ni pamoja na kuzidisha kufanya usimamizi shirikishi na mafunzo,kutoa elimu zaidi kwa jamii juu ya lishe bora.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa