- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri kupitia Idara ya Afya inaendelea kutoa na kuboresha huduma za lishe kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo
kuboresha lishe kwa jamii hasa siku 1000 za uhai wa mtoto tangu kutungwa kwani inagusa moja kwa moja kuondoa tatizo la hali mbaya ya lishe.
Halmashauri ya wilaya ya Ngara imeendelea kutoa fedha za mapato ya ndani ambapo kwa robo hii ya kwanza Julai-Septemba 2022 imetoa TSh 33,360,000/= sawana asilimia 102.
Katika robo hii ya kwanza (Julai-Septemba 2022) ya mwaka wa fedha 2022/23,Halmashauri ya Ngara ilitekeleza shughuli kama usimamizi shirikishi na kuwajengea uwezo ngazi ya jamii ambapo
wahudumu 68 waliweza kujengewa uwezo katika ujazaji wa taarifa katika fomu na upatikanaji wa taarifa hizo.Shughuli nyingine ni ufuatiliaji wa utekelezaji mwongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe elimu msingi.
Halmashauri ilijikita pia katika utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za minyoo ambapo walengwa 91081 sawa na asilimia 115.7 walipatiwa.
Shughuli nyingine ni ukarabati wa lishe ambapo watoto wote waliohudhuria walipewa chakula, dawa na kulishwa chini ya uangalizi.Mafunzo pia kwa akina mama/walezi kila siku ya darasa kuhusu usafi,
matendo changamshi kwa watoto,makundi matano ya vyakula,jinsi ya kuandaa mlo kupanga mlo na idadi ya milo kwa siku,ushirikishwaji wa
kwa akina baba katika kulea watoto,jinsi ya kujikinga na malaria pamoja na kujua faida za mtoto kupata chanjo,kupewa dawa za minyoo na kupewa dawa za nyongeza za vitamin A.
Katika kikao hicho Kaimu Afisa Lishe Ndugu Mansour Kalokola aliwasilisha shughuli zilizotekelezwa pamoja na changamoto zilizojitokeza katika robo ya nne. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Ngugu Josephat Sangatati alisisitiza ushirikishwaji wa elimu ya lishe kwa wazazi na ushirikiano udumishwe kati ya Halmashauri na wadau.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa