- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya wilaya ya Ngara imetenga zaidi ya shilingi bilioni arobaini na tisa, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, kulipa mishahara na uendeshaji wa Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, ameyasema hayo wakati wa kikao cha waheshimiwa Madiwani kilichofanyika Februari 23, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya.
“Halmashauri yetu inatarajia kupokea ruzuku ya shilingi 33,303,443,000.00 kwa ajili ya kulipa mishahara, mapato ya ndani shilingi 2,013,049,447.00, matumizi mengineyo shilingi 1,243,949,000.00 na miradi ya maendeleo shilingi 13,128,309,557.00.” alifafanua Ndugu Bahama.
Ameongeza kwamba katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, Halmashauri ilipanga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni arobaini na tano (45), lakini kufikia mwezi Disemba 2017 ilikuwa imekusanya zaidi ya shilingi bilioni kumi na tano (15).
“Waheshimiwa madiwani utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri zinaendelea kutekelezwa kwa viwango tofauti jinsi tunavyopokea fedha toka Hazina na makusanyo yanavyoongezeka.” Alisema Mkurugenzi huyo.
Rasimu na bajeti ya halmashauri ya wilaya katika mwaka wa fedha 2018/2019, inalenga kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015, kujenga uwezo wa Tehama ili kuimarisha mapato, kukamilisha ujenzi wa viporo vya maabara, kuimarisha huduma za afya na kuandaa mazingira mazuri ya kuendeleza viwanda.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa