- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Viongozi wa vikundi kumi (10) vya akina mama na vijana, vimeishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa kuhidhinisha mkopo wa zaidi ya shilingi milioni kumi na tatu (13), kwa ajili ya kuongeza mitaji ya vikundi hivyo.
Akiongea kwa niaba ya viongozi wenzake Machi 12, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri, baada ya kukabidhiwa hundi, Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Rusumo Club ndugu Deus Felician amesema; wanaishukuru serikali kwa kutambua uhitaji wao.
“Tunajishughulisha na kupanda miti ya kutunza mazingira, hivyo fedha hii itatusaidia kuongeza vitalu vya miche ya miti, ambayo tutainunua kwa ajili ya matumizi yetu na kuiuza kwa wananchi, ili tutunze mazingira.” Alisema Mwenyekiti Felician.
Aidha, amesema kwamba pamoja na mkopo waliopata; Halmashauri iliwapatia mafunzo ya ujasiliamali, aliyodai kuwa ya muhimu kwa maendeleo ya shughuli zao.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Avelina Nicholaus Kabyazi, amesema fedha waliyopata si mali ya vikundi vilivyopata mkopo huo, bali vinawajibika kuirejesha ili vikundi vingine viwezze kunufaka.
“Wale viongozi muliopita umri wa kuwa katika kundi la vijana, tafadhali achieni madalaka kwa vijana, nawaomba mtumie uzoefu wenu mlioupata kuwalea vijana wenu, ili waendeleze vikundi vyenu.” Alisema Bi Kabyazi.
Amefafanua kuwa vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni kumi (10); vya akina mama vitano (05) na vya vijana ni vitano (05), na kuongeza kuwa vikundi vinane (08) vimepokea shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=) kila kimoja, na viwili vimepokea shilingi laki nane elfu kumi na mia nane sitini na tano (810,865/=) kila kimoja.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa