- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Kwa miaka mitano iliyopita Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imepata Hati Safi ya ukaguzi kwa hesabu zilizoishia Juni 30, 2017; Halmashauri mnawajibika kuyalinda mafanikio haya, ili msirudi nyuma katika ukaguzi unaoendelea.” Aliagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja General Mstaafu Salum Mustafa Kijuu.
Agizo hilo limetolewa na mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera Meja General Kijuu Julai 25, 2018, alipokuwa akihutubia Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara katika ukumbi wa Halmashauri, kwa ajili ya kujadili taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Ameagiza Baraza la Madiwani na Manejimenti kuhakikisha wanaondoa na kuepuka kasoro zilizojitokeza katika ukaguzi uliopita; huku akiongeza kuwa ukaguzi unaonyesha kwamba Halmashauri imepata ya mashaka katika mwaka 2014/2015.
Hivyo ametoa wito Halmashauri ihakikishe inaendeleza mwenendo mzuri wa utendaji kazi; huku wakiepuka utendaji kazi wa mazoea usiozingatia taratibu, ili kuepuka hoja zisizo za lazima.
“Ninaagiza Baraza la Madiwani, kuchukua hatua zinazostahili kwa watumishi na wadau wa Halmashauri, waliosababisha kuwa na Hoja za miaka ya nyuma, ambazo majibu yake hayakumridhisha Mkaguzi.” Alisema Meja General Kijuu.
Amesema kwamba maagizo hayo yanafuatia kuwepo kwa hoja za muda mrefu, zinazoashirikia kuwepo kwa baadhi ya watendaji wa Halmashauri ambao hakutimiza wajibu wao kikamilifu.
Baadhi ya hoja za miaka ya nyuma ambazo hazijatekelezwa; amezitaja kuwa ni pamoja na mawakala kutowasilisha mapato yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30, ya mwaka wa fedha wa 2012/2013, na shilingi milioni 3,000,000/= za mwaka 2013/2014.
Aidha, amewataka waheshimiwa madiwani wahimize utelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi wachangie kikamilifu katika kukamilisha miradi ya maendeleo, iliyoanzishwa na wananchi wenyewe.
Mh. Mgata kwa niaba ya Baraza la waheshimiwa Madiwani wamemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera na kuahidi kuyateleza maagizo hayo aliyowapa na kwamba atarajie Hati Safi kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa