- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imepokea shilingi milioni 230 toka serikali kuu, kwa ajili ya kujenga madarasa manne na mabweni mawili katika shule ya sekondari ya Kabanga.
Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Aidan John Bahama, amesema hayo ofisini kwake Juni 20, 2018, kwamba fedha hiyo imetolewa na wizara ya Elimu, sayansi na Teknolojia.
“Naagiza wahasibu, na wagavi kufanya maadalizi ya kununua vifaa hivyo kutoka viwandani, ili ifikapo Julai 30, 2018, mabweni na madarasa hayo yawe yamekamilika.” Alisema Ndugu Bahama.
Ameongeza kwamba serikali imetoa fedha hiyo na imekwishaingizwa kwenye akaunti ya shule, kwa ajili ya utekelezaji, na kwamba wanaohusika wanatakiwa kuhakikisha fedha hiyo imefanyakazi iliyokusudiwa.
Naye Kaimu Afisaelimu Idara ya Elimu sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Marton James amefafanua kwamba kati ya fedha zilizopokelewa milioni 80 zitatumika kujenga madarasa ambapo kila darasa ni shilingi milioni 20.
Shilingi milioni 150 zitatumika kwa ajili ya kujenga mabweni mawili ambapo kila bweni litagharimu shilingi milioni 75, na kwamba kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80.
Shule ya sekondari ya Kabanga inawanapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita, na inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa na mabweni, kwani shule hiyo ina wanafunzi wapatao 900 wenye kuhitaji huduma ya malazi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa