- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imepokea jumla ya shilingi milioni 506 kutoka serikali kuu, kwa ajili ya kuboresha mazingira yakufundishia na kutatua changamoto mbalimbali katika shule za sekondari naza msingi wilayani humo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Gidion Mwesiga ameyasema hayo ofisini kwake Mei 05, kwamba kiasi hicho kutatumikakujenga miundombinu ya shule, aliyoitaja kuwa ni vyumba vya madarasa pamoja nanyumba za wafanyakazi.
“Kati ya shilingi milioni 506 tulizopokea; shilingimilioni 142 tutazitumia kujenga madarasa 30, shilingi milioni 153 tutazitumiakujenga maabara 09 na kiasi kinachobaki kitatumika katika shughuli za kiutawala.”Kaimu Mkurugenzi Ndugu Mwesiga.
Ndugu Mwesiga amesema changamoto kubwa waliyonayo ni kwabaadhi ya watoto ambao hawajamudu kuhesabu, kuandika na kusoma, na kudai kwamba changamoto hiyo wanaifanyiakazi, ili kuongeza ufanisi.
Ameishukuru serikali kwa kutoa vitabu vya mtaala mpya kwamasomo ya darasa la IV, ambavyo wameanza kuvisambaza katika mkoa wa Pwani, nakudai kwamba wanatarajia kuvipokea hivi karibuni.
Amewashauri wazazi wote kwa kushirikiana na kamati zashule kuwa karibu na watoto wao, ili waweze kujua maendeleo yao kitaaluma. nakuongeza kwamba Halmashauri kwa kupitia idara yake ya elimu itasimamiauwajibikaji wa walimu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa