- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imeratibu maeneo ya kuweka viwanda, kwa ajili ya kuwahamasisha wadau kuwekeza katika sekta ya hiyo.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ofisini kwake Machi 22, 2018, Mratibu wa Maendeleo ya Viwanda ndugu Syprian G. Muheranyi, amesema wametenga eneo katika kijiji cha Lwakaremela, kwa ajili ya kutimiza azma hiyo.
“Tulishawaelekeza viongozi wa kila kijiji kutenga maeneo, kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda, na zoezi la kuhakiki maeneo hayo bado linaendelea.” Alisema ndugu Muheranyi.
Hata hivyo, amsema kuwa wamebaini kuwa Ngara mjini ina viwanda 32, vyenye mtaji wa zaidi ya shilingi milioni 386, na vimeajiri wakazi wapatao155.
Amewataka wananchi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vidogo sana, kwa ajili ya kupanua fursa ya ajira na kukuza mitaji yao.
Aidha, amezitaja baadhi ya changamoto, kuwa wananchi wengi hawaelewi maana ya viwanda, malengo yake na wanavamia maeneo yaliyotengwa, kwa ajili ya kuwekeza katika sekta hiyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa