- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wanangara tulione suala la kuchangia huduma ya elimu ni letu, mwaka 2020 hatutaki mwanafunzi abaki, kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu ya darasa.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wialya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama.
Ndugu Bahama amesema wananchi wanachangishana na wanachokipata kinapelekwa kwenye ujenzi wa miundombinu shuleni, kwani kila kijiji kina shule kama siyo ya sekondari basi kitakuwa kinamiliki shule ya msingi, hivyo lazima waandae miundombinu ya shule zote.
“Na kuchangia siyo hiari ni lazima; kwa hiyo kwa mwaka huu, tutachangia tu; kwa kazi au kwa fedha, kwa ajili ya kukamilisha vyumba vya madarasa 128 vya shule za msingi, lakini na vyumba vya madarasa 48 katika shule za sekondari.” Alisema Bahama.
Halmashauri pamoja na wafanyakazi wake wamechangia takribani shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mashueni, ambapo Halmashauri imechangia shilingi milioni 24, huku wafanyakazi wote wakichangia milioni 25; Mkurugenzi shilingi 50,000/= wakuu wa idara na vitengo shilingi 20,000 kila mmoja, wafanyakazi shilingi 10,000 pamoja na wahudumu shilingi 5,000/=.
Amesema shule zote wanaeendelea na ujenzi, na kudai kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Ngara haikuwa na upungufu mkubwa; wanahamasisha wananchi wajenge vyumba vya madarasa vinavyopungua mwaka huu; wakilenga upungufu wa madarasa ya wanafunzi watakaoingia mwaka 2020.
Amezitaja madarasa saba yaliyopungua kwamba yanajengwa katika shule za Nyakisasa, Rusumo ‘B’, Kanazi, Mugoma, pamoja na Mabawe, ambapo hata hivyo mapungufu ni kidogo, “lakini tunashukuru kote mambo yanakwenda vizuri.” Alisema Ndugu Bahama.
“Katika maandalizi ya vyumba vya madarasa; sisi tuko vizuri kwa sababu tunatakiwa kujenga madarasa saba, lakini katika ziara niliyoifanya ya Januari 13, 2019 nimekuta vyumba vingi viko kwenye renta na tunatarajia mwezi ujao kama tarehe 15, 2019 vyumba hivyo viwe vimekamilika.” Alisema Ndugu Bahama.
Halmashauri kwa sasa inahamasisha kila kijiji kiwe na benki ya tofali 300,000 kwani tafali laki tatu mara vijiji sabini na mbili itakuwa tofali za kutosha, kukomesha tatizo la upungufu wa miundombinu mashuleni.
Kapeini hiyo, itazinduliwa rasmi Machi 30, 2019 ili kupisha kwanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na masomo yao ifikapo Machi 15, 2019; baada ya hapo itaanza kujenga madarasa mengine ya kupokea wanafunzi wa mwaka 2020.
Baadhi ya vijiji vimekwishaanza kujenga vyumba vya madarasa kwa ajili ya kupokea wanafunzi watakaoingia awali, darasa la kwanza pamoja na wa kidato cha kwanza mwaka 2020, ambazo amesitaja kuwa ni shule ya Kibimba inaendelea na ujenzi wa madarasa 02 yamefikia renta.
Shele nyingine ni Rusumo ‘B’ darasa moja linakaribia kwenye renta, ambapo shule nyingine za msingi na za sekondari nao wanaendelea na ujenzi wa miundombinu hiyo; huku akisema kwamba shule za sekondari wanaupunfu wa vyumba 48, lakini vinavyojengwa 34 kwa hiyo upunfu madarasa 14.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa