- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kupitia Idara ya Elimu Msingi, imetumia wiki ya elimu kuhamasisha jamii kutambua umuhimu na kuongeza ari ya utendajikazi kwa walimu na wanafunzi wilayani humo.
Akisoma risala wakati wa Hitimisho ya Wiki ya Elimu kwa niaba ya Afisaelimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mei 30, 2018, Afisa Taaluma (W) Ndugu Oswald Rujuba, amesema wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuinua taaluma ya wanafunzi wilayani Ngara.
Amesema maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Elimu yamesimamiwa na idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari na kwamba idara ya Elimu Msingi katika wiki hiyo imefuatilia maendeleo ya taaluma katika shule ya za msingi zipatazo 74.
“Kutokana na hali ya taaluma wilayani kwetu kushuka; tumetoka nafasi ya 01 hadi ya 08 kimkoa, tuliamua kufanya maadhimisho haya kwa kutembelea shule moja, ili kuhamasisha na kuongeza ari ya utendajikazi kwa walimu na wanafunzi wajisomee kwa bidi.” Alisema Afisaelimu Taaluma ndugu Rujuba.
Katika risala yake ameihamasisha jamii, kuwekeza katika Elimu kama hatua muhimu ya kuzalisha nguvu kazi yenye ujuzi wa kulisaidia taifa lao, na kuongeza kwamba uhamasishaji huo, umepelekea ofisi yake kuongeza idadi ya wanafunzi 84,125 waliosajiliwa.
Amefafanua kwamba idara ya msingi imefanya vizuri kitaaluma, ambapo katika mitihani ya darasa la VII kitaifa kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 hadi 2017, imekuwa ya kwanza kimkoa na imefanikiwa kuvuka lengo.
Maadhimisho ya siku ya kilele cha wiki ya Elimu yameabatana na kuwatunuku vyeti walimu wakuu, ambao shule zao zimefanya vizuri kitaaluma, ambapo shule tano za sekondari na tano za msingi wametunukiwa vyeti hivyo.
Idara ya Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara inazo shule 121, shule 115 ni za serikali, ambapo shule 06 ni za watu binafsi, na kwamba idara yake ina walimu 1,373; walimu wa kiume ni 867 na wa kike 506.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa