- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kipindi cha robo ya tatu Idara ya Elimu Sekondari kupitia shule za sekondari 23, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imepokea shilingi 171,139,189.00 kwa ajili ya elimu bila malipo, katika kipindi cha Julai hadi Machi 2018.
Kaimu Afisaelimu idara ya elimu sekondari Ndugu Marton James, amedhihirisha hayo wakati wa kikao cha robo ya tatu, kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Aprili 2018, katika ukumbi wa Halmashauri.
Amechanganua kwamba katika kipindi hicho, idara yake imepokea jumla ya shilingi 25,425,297.00, ikiwa ni fedha ya fidia ya ada kwa shule za kutwa, ambapo shilingi 115,528,416.00, zimetolewa kwa ajili ya kununua chakula kwa wanafunzi wa bweni.
“Pia tumepokea shilingi 18,685,476.00, ili zitumike kwa ajili ya uendeshaji, ambapo shilingi 11,500,000.00, tumezipokea na tumelipa wakuu wa shule za sekondari posho ya madaraka.” Alisema Ndugu James.
Kaimu huyo wa elimu sekondari Ndugu James, ameishukuru serikali kwa kupeleka fedha ya elimu bila malipo kwa wakati, kwa sababu hiyo shule 23 za sekondari wilayani humo, zimefanikiwa kuendesha shule hizo kwa urahisi.
Aidha, ameongeza kwamba idadi ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika mwaka 2018, imeongezeka kutoka 3826 hadi kufikia wanafunzi 3288.
Kaimu huyo wa sekondari hakusita kutanabahisha kwamba, idara yake ina upungufu wa walimu wa sayansi hasa wa hisabati, na wataalamu wa maabara na kwamba jumla ya maabara 69 hazijakamilika ujenzi wake, kwani ni zimekamilika maabara 22 tu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa