- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imefanikiwa kukopesha vikundi vya akina Mama na Vijana shilingi milioni 30,000,000/= katika mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Hayo ni kwa mujibu wa Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Josephine J. Lusatira, alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake Agosti 13,2018, kwamba Idara yake imekwisha toa mikopo tajwa kwa walengwa hao.
“Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, makadirio ya makusanyo ya Halmashauri kwa mwaka, yalikuwa shilingi 1,035,005,000/=, na kutoa asilimia 10% ya T.shs. 103,500,500/= kwa vikundi vya wanawake na vijana.” Alifafanua Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Josephine J. Lusatira.
Makusanyo halisi hadi Juni 30, 2018 ilikuwa T.shs. 930,708,085.20, ambapo asilimia 10% ni T.shs 93,070,808.52 na kwamba Marchi, 2018, walikopesha shilingi 13,621,730/= kwa vikundi 10, vikundi 05 vya vijana vilikopeshwa shilingi 6,810,865.00 na vikundi 05 vya wanawake shilingu 6,810,865.00 sawa na asilimia 16.8%.
Mwishoni mwa mwezi Juni, 2018, idara yake ilikopesha vikundi 08 shilingi 16,378,270/=, ambapo vikundi 02 vya vijana vilipokea shilingi 5,000,000/= na vikundi 06 vya akina mama vilikopeshwa shilingi 11,378,270/=.
Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali, ambazo halmashauri inakumbana nazo katika kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake, ambazo ameainisha kuwa ni ufinyu wa bajeti na makusanyo kidogo ya halmashauri.
Amesema ufinyu huo husababisha idara ya Maendeleo ya Jamii, kushindwa kuvifuatilia vikundi vilivyopewa mikopo, kwa ajili ya kutoa ushauri na kuhamasisha kurejesha mikopo katika muda uliopangwa.
Amesema baadhi ya vijana ugawana fedha za mikopo, walizopewa kwa matumizi mengine, na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, na kwamba baadhi ya wakopaji wanahamia nje ya wilaya, kwaajili ya utafutaji bila kurejesha mikopo waliyochukua.
Aidha, amesema Idara yake imeboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani, ili kuongeza kipato na kuweza kutoa 10% ya mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.
Idara inaendelea kufanya ufuatiliaji kwa vikundi vya vijana na wanawake, vilivyochelewa kurejesha mikopo waliyopewa ili kuwezesha vikundi vingine.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa