- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakuu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kuimarisha idara za kila somo na kuhakikisha kila mwanafunzi anafaulu somo la idara husika, hasa masomo ya sanaa yenye ambayo yana walimu wakutosha.
Afisaelimu Idara ya sekondari katika Halmashauri hiyo Ndugu Fikeni Ezekiel Senzighe, ameyasema hayo ofisini kwake Februari 11, 2019 kwamba kila idara iwiwe kumfuatilia kila mwanafunzi katika matokeo yake, ili wanafunzi hao waweze kufanya vizruri.
“Kila idara itoa mazoezi ya kutosha, ili kila mwanafunzi apate A na B katika masomo ya sanaa; kwa masomo ya sayansi, ambayo yana uhaba wa walimu; walimu wawe wana wanatoka shule moja kwenda nyingine kufundisha masomo hayo, kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao.” Alisema Ndugu Senzighe.
Lakini wakuu wa shule watakaoweza kuwaajiri walimu wa muda wa masomo ya sayansi, wamewaruhusiwa kufanya hivyo, ili lengo la kufaulisha kwa asilimia 100%; kwa kutumia walimu wa sayasi waliopo ili kuziba pengo lililopo.
amesema katika mwaka wa masomo wa 2019 wameweka mikakati ili kuhakikisha ufaulu uwe daraja la kwanza hadi la tatu; aidha, huku wakinuia kuondoa daraja la sifuri katika matokeo ya mwaka 2019.
Mikakati mingine waliojiwekea ni kuwashirikisha wazazi mara kwa mara katika vikao vinavyoendelea, ili kuhakikisha wazazi wanawapa watoto mahitaji muhimu ya shule, sare za shule, daftari, kalamu, chakula cha mchana au uji wawapo shuleni.
Kubwa waliloazimia ni kuimarisha nidhamu ya wanafunzi shuleni, ili shuleni pawe ni mahali pa kujifunza zaidi, na siyo mahala pa kutoa adhabu mara kwa mara, na kufuatlia makosa madogo madogo ambayo hayana tija kwa wanafunzi.
Wametembelea shule moja hadi nyingine, ili wajionee jinsi watoto walivyoripoti, na namna walimu walivyojipanga kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, na kuwatia moyo pale, kuimarishaa nidhamu ya wanafunzi, na washirikiana na wazazi, ili kuimarisha nidhamu ya wanafunzi shuleni.
Kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana au uji mshuleni, lakini pia na walimu wahakikishe wanapata chai nzito au chakula pale mazingira yatakaporuhusu, ili waweze kufundisha wakati wa ziada huku wakiwa na nguvu.
“Lakini kubwa zaidi, tulikazia kuwepo na kamati ya taaluma kwa kila shule, isimamie ufundishaji, maadalio na ufundishaji wa kila siku, mazoezi ya asubuhi, mazoezi ya kila wiki, mitihani ya kila mwezi, ya mihula; tukiagiza mithani hiyo iwe na viwango.” Alisema Ndugu Senzighe.
Amesema wamegundua kwamba matokeo hayakuwa mazuri kwa sababu ya ulegevu katika usimamizi katika ngazi ya shule na ya kata; kwa hiyo, wanafuatilia shule hizi kwa kuongea na walimu, ili kurekebisha yale ambayo hayafanyiki inavyotakiwa.
Amezitaka shule zilizofanya vibaya kila mwalimu hakikishe anatekeleza wajibu wake ipasavyo, ili aweze kuziba mapungufu yaliyojitokeza na atakayeshindwa kufanya hivyo, basi italazimika atafute sehemu nyingine.
Matokeo ya Kidato cha IV kwa mwaka 2018 siyo mazuri na wala siyo mabaya, yamekwenda kinyume na matazamio yao, kwani lengo lilikuwa ni kufaulisha daraja la kwanza hadi la tatu kwa 50% lakini wamafaulisha kwa 36.7%.
Kitaifa wilaya ya Ngara imekuwa ya 86 katika matokeo ya kidato cha IV mwaka 2018, ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2017 ambapo wilaya ilishika nafasi ya 84 kitaifa, kwa hiyo imeshuka kwa pointi mbili.
“Kimkoa mwaka 2018 Wilaya ya Ngara imeendelea kushikiria nafasi ya 03, kama tulivyokuwa tumeshika nafasi hiyo mwaka 2017, na kufaulu kwa shule zetu katika Halmashauri yetu kumejigawa katika shule za binafsi na za serikali.” Alisema Afisaelimu huyo.
Amesema shule za binafsi zimefanya vizuri zaidi kwani shule tano zimeongoza, alizozitaja kuwa ni Rulenge, Precious, Lake St. Joseph Mbuba na Baramba Girls kwa kutokuwa na sifuri, ambapo shule za serikali zilizofanya vizuri ni Mluvyagira, Murusagamba, na Muganza.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa