- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanufaika wa mfuko wa akinamama, vijana na walemavu katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara, wametakiwa kuimarisha uongozi wa vikundi na kuinua kipato chao, kabla ya kuomba fedhaya mkopo toka katika mfuko huo.
Wito huo umetolewa na wanakikundi mbalimbali, waliotembelewa na idara ya Maendeleo ya Jamii Wilayani Nagra, ili kujiridhisha na uwepo wa vikundi vilivyoomba mkopo, kabla ya kutoa fedha kwa vikundi hivyo, Mei 08, 2019 katika kata za Rusumo, Nyakisasa, Rulenge na Kabanga.
“Wanakikundi wengi wanashindwa kurejesha mikopo waliochukua, kwani uongozi usiokuwa imara, unashindwa kuwaimiza wanakikundi, kurejesha mikopo yao kwa wakati ikizingatiwa kuwa maisha ya wanakikundi hao ni duni.” Alisema Ndugu Audax Alex mwanakikundi cha Rusumo Bodaboda Group.
Ndugu Alex amesema kutokurejesha fedha ya mkopo kwa wakati maana wanamaanisha kwamba viongozi wao watiwe hatiani, kwani kila mmoja anajua kwamba fedha ya mkopo siyo zawadi lazima irejeshwe kwa wakati, ili vikundi vingine.
Naye Valerian Audax amefafanua kwamba kikundi chao cha Bodaboda Group kimefanikiwa kurejesha fedha yote waliokopa kwa wakati kwa sababu ya kuwa na uongozi thabiti, huku kila mmoja akitimiza wajibu wake kwa kuhakikisha fedha hiyo imeufikia huogozi wao kwa wakati muafaka.
Akieleza jinsi walivyonufaika na mkopo wa akinamama, vijana na walemavu, Ndugu Audax amesema fedha waliyopata imewasaidia kukuza kipato chao kwani kutegemema bodaboda pekee haitoshi, kwani wakati wa mvua hawapati wateja wa kutosha, lakini kwakuzungusha fedha hiyo wameinua maisha yao.
“Tulitumia fedha hiyo kama mtaji wa kipato cha ziada, baada ya kupata hiyo fedha nilimpatia mke wangu ambaye aliitumia kuuza mboga na samaki; kwa kweli imenisaidia kwani wakati huu wa mvua hatupati wateja wa kutosha katika shughulizaetu za bodaboda.” Alisema ndugu Audax.
Bi. Juliana Tumaini wa kikundi cha Umoja ni Nguvu wa kijiji cha Kashinga katika kata ya Nyakisasa, amewashauri wanavikundi katika Wilaya ya Ngara kutumia mikopo wanayopokea katika malengo waliyoeleza wakati wa kupata mkopo, kwani wengi wamekuwa wakikiuka malengo yao na kufanya kinyume.
Aidha, Bi. Tumaini amesema wao, wamefanikiwa kurejesha fedha hiyo, kwa sababu wameitumia katika malengo waliyojiwekea na kuelewana; na kuongeza kwamba kuelewana huko kunaondoa tofauti zao.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Avelina Kabyazi, amewashukuru wanakikundi waliorejesha fedha hiyo kwa wakati, na kuwasistiza kuepuka udanganyifu aliosema umeshamiri miongoni mwa wanakikundi wengi.
“Kutorejesha fedha hiyo kwa wakati ni kujizuilia faida wenyewe; kwani mtafungiwa kupewa mikopo, mtaawakwamisha wanavikundi wengine kupata mkopo kwa sababu fedha, ambayo ingezunguka kwa wanavikundi hao, inakuwa mikononi mwa wachache wasiokuwa waaminifu. Alisema Bi. Kabyazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imekuwa ikitenga asilimia 10 kila mwezi, kutoka katika mapato yake ya ndani, kwa ajili ya kutoa mikopo kwa akinamama, vijana na walemavu, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa