- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walengwa wa malipo ya dirisha la kipindi cha Septemba – Oktoba 2018 wa TASAF III katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwa nasubira wakati mchakato wa malipo yao unakamilishwa.
Afisa Ufuatiliaji Mradi wa TASAF III Ndugu Frank L. Anthony, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imepokea jumla ya shilingi 279,660,500.00 kwa ajili ya malipo ya ruzuku kwa kaya masikini na uwezeshaji wa zoezi hilo.
“Tumepokea shilingi 259,700,000.00, kwa ajili ya ruzuku kwa kaya maskini zipatazo 7748 kutoka katika vijiji 52 vilivyo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini - TASAF III, zoezi hili litaaanza mara tu taratibu za kifedha zitakapokamilika.” Alisema Ndugu Anthony.
Aidha, katika kiasi kilichopokelewa, shilingi 5,200,000.00; zitatumika kwa ajili ya uwezeshaji wa malipo ngazi ya kijiji, ambapo kila kijiji kitapokea shilingi 100,000.00 kama malipo kwa wenyeviti, watendaji, wajumbe watatu ngazi ya kijiji pamoja na mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi ngazi ya jamii (CMC).
Ndugu Anthony amesema kiasi cha shilingi 13,980,500.00, kitatumika kwa ajili ya kuwezesha zoezi la kuhawilisha fedha kutoka Halmashauri kwenda katika kila kijiji kulichomo katika mpango.
Alifafanua kwamba kiasi cha shilingi 780.000.00, kitatumika kuwezesha shughuli za mpango na zoezi la malipo ngazi ya kata, ambalo linawahusisha waratibu elimu kata, maafisa ugani na wauguzi wanaohusika kujaza fomu za masharti ya afya kwa walengwa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa