- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kujitokeza kwa wingi, wapate elimu katika sekta ya utalii, ili waweze kuinua kipato chao, lakini na serikali iweze kupata mapato yake.
Hayo ni Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama ofisini kwake April 30, 2019, kwamba Halmashauri ina dhamana ya kuwaandaa wananchi wake, ili waweze kuingia katika uchumi huo wa kitalii.
“Wilaya ya Ngara inakwenda kuingia katika biashara ya kitalii, lakini katika uwekezaji nimeona ni busara Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ina vijana, ambao wanaweza kufanyakazi katika eneo hili la utalii, nimeona niwaandae kwa fursa hiyo, wasiweje kuwa wasindikizaji.” Amesema Ndugu bahama.
Kwa sasa ninaandaa Halmashauri imeandaa programu, ambayo itakuwa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na vyuo vya kitalii vya Musoma Utalii College kilichoko Tabora na Arusha Utalii College kilichoko Arusha kwa lengo la kuwaandaa wananchi, kutumia fursa inayoletwa na hifadhi ya Burigi.
Katika kufanikisha azma hiyo, amewasiliana na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera ambaye ameridhia na kukubariana na wazo hilo, na kuongeza kwamba tayari wamefanya mazungumzo ya awali na vyuo hivyo, ambayo watayakamilisha mwezi Mei 2019.
“Mipango itakapokamilika vitakuwa na dhamana ya kuja kuwafundisha wananchi wetu hapa wilayani Ngara, kwa sababu natambua watu wengi hawana uwezo wa kwenda kusoma kwenye vyuo hivyo, na wenye uwezo hawana muda wa kwenda vyuoni.” Amesema Ndugu Bahama.
Kwa matakwa ya Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ay Ngara, wananchi waanze kusoma kazi fupi fupi, zitakazo wawezesha kuufahamu utalii, lakini kuwandaa kuingia katika soko la utalii
Kwa upande wa wafanyabiashara anapendekeza wawe na elimu ya jinsi ya kujenga hoteli, kambi za kupokelea watalii na vituo vya habari na mawasiliano, huku akiwataka vijana kujifunza kozi za Hotel Management, Hospitality, Tour guards pamoja na potters, wakiyajua watapata ajira.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Erick Nkilamachumu, amesema kwamba hifadhi ya Burigi kuwa mbuga za wanyama, itapelekea kukua kwa uchumi wa wilaya zinazozunguka Mbuga hiyo.
Amezitaja Wilaya hizo kuwa ni Ngara, Biharamulo, Muleba na Karagwe; ma kwamba ni matumaini yao kwamba katika siku za usoni uchumi wa wana Ngara utapanda, huku akiwataka wananchi kujipanga kutumia fursa hiyo kwa kuandaa mazingira mazuri.
Pamoja na hayo, amewakumbusha wananchi, wajiadae kwa kuongeza uzalishaji ikiwa ni pamoja na kulima mazao ya chakula nay a biashara kwa ajili ya wageni watakaoitembelea Wilaya ya Ngara.
“Siyo wakulima tu, bali hata wafanyabisahara, wataweza kuongeza kipato chao kwa kuuza vitu vyao, lakini kinachotakiwa ni wafanyabisahara hao kujipanga, ili wahakikisha bidhaa zote muhimu, zinapatikana na katika ubora unaotakiwa.” Alisema Nkilamachumu.
Diwani wa Kata ya Murusagamba Wilaya Ngarani Ndugu Soud Mukubira amesema kwamba suala la utalii katika wilaya ya ngara ni fursa kwa wananchi hasa vijana wao, ambao watapata mafunzo, na hatimaye inawezekana wakapata ajira.
“Kwetu sisi, hiyo ni fursa kwa sababu utalii umekuwa katika wilaya na mikoa ya mbali, lakini kwa sasa tumepata nafasi ya kuingia katika mzunguko wa utalii; kwa hiyo tutaweza kutembelea mbuga hizo ndani ya wilaya ya yetu.” Alisema Ndugu Mkubira.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa