- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ujumbe wa Kitaifa wa Maafisa wa Vyombo Mbalimbali vya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence Collage) ukiwakilisha nchi 11 wameutembelea Mkoa wa Kagera kujifunza na kubadilishana ujuzi katika masuala ya Ulinzi na Usalama.
Ujumbe huo umefanya mafunzo hayo mkoani Kagera Januari 7, 2019, ambapo pamoja na kubadilishana ujuzi na uongozi wa Mkoa katika masuala ya Ulinzi na Usalama, wametumia fursa hiyo kushauriana njia stahiki za kukuza uchumi Mkoani humo.
Maafisa 16 kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa ukiwa na Maafisa kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Nigeria na China mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera, ulipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake.
Akieleza lengo la safari yao, Kiongozi wa Ujumbe huo Balozi Peter Kallage, alisema wamekuja kuja Mkoani Kagera, kujifunza na kubadilisha mawazo katika Nyanja za ulinzi na usalama kimataifa na kuona namna bora ya kuendeleza fursa mbalimbali za kukuza uchumi mkoani humo.
“Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kipo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na kinaendesha kozi mbali mbali za Kimataifa kama unavyoona; hapa tuna Maafisa kutoka nchi nne kama nilivyozitaja hapo awali, lakini kwa kozi hii, ambayo imetuleta hapa Kagera ina Maafisa kutoka nchi 11 na tumewagawanyika katika makundi 04, weninge wamekwenda katika mikoa mingine sisi tumechagua kuja Kagera.” Alifafanua Balozi PETER KALLAGE
Ujumbe huo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa ulipitishwa kwenye Wasifu wa Mkoa wa Kagera wa Kiuchumi na Kijamii, ili kuonesha maendeleo ya Mkoa, Fursa mbalimbali za uwekezaji na changamoto katika kukuza uchumi wake na uchumi wa wananchi kwa ujumla.
Katika wasilisho hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti, alisema kuwa pamoja na Mkoa wa Kagera kufanya vizuri kiuchumi; lakini changamoto kubwa ni Wahamaiaji Haramu, na Biashara ya magendo ya Mazao.
“Pamoja na Mkoa wetu kuwa na fursa nzuri za kiuchumi kwa kupakana na nchi tatu za Rwanda, Burundi na Uganda na kuwa kitovu cha biashara cha Jumuiya ya Afrika Mashariki; lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya Wahamiaji haramu na Biashara ya Magendo ya mazao. lakini tunapambana nao.” Alieleza Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Amesema kwamba pamoja na changamoto hizo wanaendelea kushirikiana na viongozi wenzao wa nchi jirani kukomesha uhamiaji haramu, pia uongozi wa Mkoa umeanzisha Mkakati wa Nyumba Kumi bora ukilenga kukomesha biashara hiyo.
Maafisa hao mara baada ya kupitishwa kwenye Wasifu wa Mkoa walishauri namna ya kuimarisha Ulinzi na Usalaama katika Mkoa, na namna bora za kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Kagera, ili kuinua uchumi wa mkoa huo na kuchangia pato la Taifa.
Kiongozi wa ujumbe huo aliushukuru Uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kukubali ombi la chuo hicho, kuuleta ujumbe wa Maafisa hao Mkoani Kagera, kujifunza fursa mbalimbali za Kiuchumi, kiulinzi na kiusalama na kuona fursa za uwekezaeji zilizomo Mkoani humo.
Aidha, ujumbe wa Maafisa 16 kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa utakuwepo Mkoani Kagera siku saba, kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji, utalii, viwanda na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali Mkoani Kagera.
Na: Sylvester Raphael
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa