- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Haki ya Mungu ninawaambia; kama uliteuliwa Afisaelimu kata au Mkuu wa shule kwa lengo la kupumuzika na siyo kusimamia taaluma, urejeshe barua ya uteuzi wako, maana unaondoka muda si mrefu.” Alisema Afisaelimu wa Mkoa wa Kagera Ndugu Alyce Kamamba.
Ndugu Kamamba ametoa rai hiyo, akiongea na Mafisaelimu, wakuu wa shule, walimu wa Taaluma wa shule za sekondari na za msingi mwezi April 2019, kwamba viongozi katika sekta ya elimu, imewapasa kusimamia majukumu yao, ili kuinua taaluma mkaoani humo.
“Ukicheza na nyani unakula mabuha, maafisaelimu mkicheza naanza na ninyi; watumieni walimu mlionao kuinua taaluma mkoani Kagera, na anzeni kuwachuje wazembe kwa kuangalia shule za mwisho katika matokeo.” Alisema Ndugu Kamamba.
Amesema kwa mujibu wa nafasi mbalimbali katika sekta ya elimu, kila mwaajiriwa ana majukumu yake, lakini baadhi yao hawatimizi wajibu wao inavyotakiwa, Akitoa mfano, amesema kuna baadhi ya wakuu wa shule kazi yao ni kuzunguka na cheki tu huku kazi vituoni kwao zikilala.
Msimamizi huyo wa Elimu Mkaoni Kagera, ameagiza kila shule iwe na kamati ya taaluma, ambayo itamsaidia mkuu wa shule, kupitia maswali ya mitihani, ili kuona kama ni ya viwango vinavyokubalika.
Pia, amewataka kuanzisha ‘clubs’ za masomo na za mazingira, shuleni na kuwataka kuzitumia kikamilifu, ili kuboresha taaluma na mazingira ya shule, ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya matunda na ya vivuli.
Mkoa wa Kagera mwaka 2019 umejipanga kutopoteza mtoto, kwa hiyo watoto walioandikishwa kujiunga shule ya sekondari au ya msingi, lazima wamalize masomo yao ya darasa la VII, na wa sekondari lazima wamalize kidato cha IV au cha VI, kwa ufaulu wa 100%.
“Ili tuhakikishe kwamba tunaondoa daraja la IV na 0, nimeelekezwa na mkoa ifikapo tarehe Augost 30, 2019, kila mwalimu awe amemaliza mada zake tunaanza marudio; ukibaki na mtoto ambaye amefeli huyo ni wa kwako, na utajua pa kumpeleka.” Alisema Ndugu Kamamba.
Amwaagiza maafisaelimu, kuhakikisha mkoa unafaulisha wanafunzi kwa asilimia zote, na hakuna mtoto hata mmoja anayepotea, na kuwataka wawatumie walimu waliona kwani walimu wa masomo ya sanaa wapo wa kutosha, shida ni ya walimu wa masomo ya sayansi.
Kuhusu watoro, ameagiza walimu wakuu kupitia bodi na kamati za shule kutumia sheria ya elimu, kwamba mtoto akikosa shule kwa siku 90, kama alikuwa mgonjwa anapewa barua ya kukariri, na kama ni mtoro aondolewe kwa mujibu wa sheria iliyopo.
“kwa hiyo wewe mkuu wa shule kazi yako ni kuwasiliana na vyombo vya serikali kudhibiti utoro, mtoro amethibitika aonekani shuleni, tunamuondoa kwa mujibu wa sheria iliyopo.” Alisema ndugu Kamamba.
Kikaokazi hicho kinafuatia ratiba aliyojipangia Afisaelimu Mkoa ya kuwahamasisha walimu katika ufundishaji na ujifunzaji, huku akiwapongeza kwa kazi nzuri ya kuadibisha, na kuwafundisha watoto wa taifa hili.
“Nilianza na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, na baadae nikaja Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, nako nimefanyakazi kwa siku kadhaa, leo niko Halmashauri ya wilaya ya Ngara, baada ya hapa nitaendelea na Halmashauri zilizobaki.” Alisema Msimamizi huyo wa Elimu Mkaoni Kagera.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa