- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya fedha,utawala na Mipango imetembelea ujenzi wa jengo la makao makuu ya halamshauri ya Wilaya ya Ngara. Katika ziara hio,mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Wilbard Bambara amemtaka mkandarasi wa jengo hilo kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.
Aidha Waheshimiwa madiwani wamewataka wakandarasi kuzingatia kanuni za usalama katika mradi ili kuondoa uwezekano wa ajali mbalimbali zinazotokana na kukosekana kwa elimu ya usalama katika eneo la ujenzi.
Mratibu wa mradi wa LADP ambao ndio mfadhili wa mradi huo amsema ujenzi unatarajia kukamilika mapema mwaka 2024 na mpka sasa mkandarasi anaenda vizuri na mkataba na anazingatia muda.
Ujenzi huu ukikamilika utafanya ofisi zote za Halmashauri kuwa eneo moja na kufanya huduma kupatikana sehemu moja tofauti na sasa ambapo ofisi za halmashuri hazipo pamoja na hivyo kufanya upatikanaji wa huduma kuchukua muda.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa