- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa kagera Leo tarehe 28/01/2024 Imetembelea Miradi ya Maendeleo Wilayani Ngara.
Kamati hiyo ambayo imeongozwa na M/kiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa kagera Alhaj Naziri Mustapha Karamagi akiwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Christopher Pallangyo katibu itikadi na uenezi Mkoa Comred Hamimu, akiwemo Mjumbe wa Kamati hiyo Toka Ngara Mhe Issa H.Samma, Bi Hajatt Faidha kainamula Wajumbe wengine na sekritaliety ya CCM Mkoa na viongozi wa Chama na serikali.
Ambapo ngazi ya Wilaya ilikuwa na Bi Hatujuani Ally Lukali katibu Tawala Wilaya aliyewakilisha Mhe Mkuu wa wilaya, Mkiti wa CCM Wilaya Comred Vitalis Ndailagije, katibu wa CCM Wilaya Bi Anastazia A. Amas mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba Ruhoro, Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wibard Bambara, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya,Waheshimiwa Madiwani , kamati ya usalama , Wakuu wa Idara na vitengo na uongozi wa LADP.
Miradi iliyotembelewa ni
1. Ujenzi wa shule Mpya ya Nyaihanga iliyojengwa Kwa thamani yaTsh 348,500,000.00 = kupitia programu ya BOOST.
2. Kituo Cha Afya Lukole ambapo gharama iliyopangwa katika utekelezaji Mradi huo TShs 729,379,882.00 = na Mradi umekamilika pia kituo hicho kilipokea vifaa vyenye thamani ya Tsh 301,746,000.00=
3. Ujenzi wa miundombinu ya kidato Cha tano na sita Ngara high school ambapo Gharama ya Mradi ni TShs 613,100,000 pia Mhe Mkiti wa CCM Mkoa wa kagera Alhaj Karamage alitoa Tsh 1,000,000.00/ = Kwa wanafunzi kwa kufurahishwa fedha hiyo alikabidhiwa Mkuu wa shule hiyo.
4. Mradi kubwa wa maji Rusumo Wenye thamani ya Tsh 3,047,641,964.59 ambapo mkandarasi ameshalipwa TShs 2,607,338,670.00 na kiasi kilichobaki kitalipwa baada ya kumalizika muda wa matazamio .Mradi huo umefadhikiwa na Benki ya Dunia kupitia wakala wake NELSAP ( Nile Equatorial lake Subsidiary Action program).
5. Kituo Cha Afya Rusumo chenye thamani ya Tsh 1,500,825,132.70 pia kilipokea vifaa vyenye thamani Tsh 268,034,000.00/=.
6. Ofisi ya ccm Kata Ya Kasulo ambapo Mkiti wa CCM Mkoa aliweka jiwe la Msingi na kuwachangia Tsh 1,000,000,00/=
Ziara hiyo ya Kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo Ikiwa ni sehemu Kabla ya uzinduzi wa maadhimisho ya kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi
Aidha Mwisho Mkiti wa CCM Mkoa Alhaj Naziri M. Karamagi na timu ya viongozi wa Chama na serikali walihudhuria sherehe za uzinduzi wa maadhimisho kimkoa Kata ya Kasulo( Benaco ) Wilayani Ngara ambapo alihutubia akimpongea Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta fedha nyingi ambapo wamejionea Miradi mikubwa mizuri yenye fedha nyingi. Alhaj Karamagi alimalizia Kwa kuwajulisha kuwa kilele Cha sherehe za CCM Mkoa zitafanyika Wilayani Muleba.
Mkiti wa CCM Mkoa wa kagera akiongoza timu aliyoambatana nayo Kutembelea Mradi wa shule Mpya ya Msingi Nyaihanga iliyopokata ya Kasulo Wilayani Ngara.
Darasa la Awali shule ya Msingi Nyaihanga.
Mjumbe wa kamati ya siasa CCM Mkoa Mhe Issa H.Samma akiwa wamekalia Dawati ndani ya Darasa na Afisa elimu Mwl Enock Ntakisigaye.
Kituo Cha Afya Lukole.
Mkiti wa CCM Mkoa na timu yake wakiwa kituo Cha Afya Lukole.
Mkiti wa ccm Mkoa akiongozwa kutembelea Shule ya Ngara high school Bi Hatujuani A. Lukali katibu Tawala wilaya Kwa niaba ya Mhe Mkuu wa Wilaya.
Mkiti wa CCM Mkoa aliongea na wanafunzi wa Ngara high school na akitoa tsh Milioni moja.
Kituo Cha Afya Rusumo ambacho kimetembelewa na kamati ya siasa CCM Mkoa.
Kituo Cha Afya Rusumo.
Yakitolewa maelezo ya kituo Cha Afya Rusumo Kwa kamati ya siasa CCM Mkoa.
Mradi wa maji Rusumo Wilayani Ngara.
Viongozi wakiwa Mradi wa maji Rusumo na kupewa maelezo ya Mradi Ambao imeanza kufanya kazi.
Mradi wa maji Rusumo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa kagera akitembelea Mradi mkubwa wa maji Rusumo.
Wananchi walivyojitokeza katika uzinduzi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa