- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kaimu Afisa Mipango wa wilaya Ndg Ghalib Idd Mkumbwa ameziasa kamati za Ujenzi, Manunuzi na Mapokezi kushirikiana wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Aliyasema hayo tarehe 9 Februari 2018 Katika kituo cha Afya cha Murusagamba wakati akizungumza na kamati hizo zinazohusika na ujenzi wa Wodi ya akina mama, Chumba cha upasuaji, OPD, Nyumba ya mganga Mfawidhi na Chumba cha kufulia ambavyo vitagharimu Tshs milioni 400.
Aidha, Diwani wa kata ya Murusagamba Mh. Mkubila S. Soud, akiongea katika kikao hicho alieleza kuwa ameshafanya mikutano na wananchi katika kata yake kuhamasisha nguvu za wananchi katika ujenzi huo unaotarajiwa kuwa umekamilika ifikapo tarehe 30 Aprili 2018.
Sambamba na ujenzi huu, ujenzi mwingine wa kiasi kama hicho cha fedha unaendelea katika kituo cha Afya cha Mabawe, kata ya Mabawe, tarafa ya Kanazi.
Hatua mbalimbali za ujenzi katika picha
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa