- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ofisi ya Mganga mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya imeamua kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi wa Ngara kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii yani CHF na pia kuchangia duka la dawa la wilaya. Mganga mkuu kwa kushirikiana na baadhi ya wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi wanapita katika kila kaya ili kufanikisha zoezi hili. Katika kata zote ambazo wamepita mganga mkuu amekuwa akitoa maelezo kuhusiana na mfuko wa Bima ya afya, umuhimu wake na dhana nzima ya uanzishwaji wa duka la dawa la wilaya. Katika maelezo yake mganga mkuu amesema kwamba pesa inayotakiwa kuchangwa kwa mwanachama anaetakakujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii na kuchangia duka la dawa ni shilingi elfu kumi na tano (15,000). Elfu kumi itabaki katika kituo cha afya, zahanati ama hospitali kwa ajili ya Bima ya afya na elfu tano itaenda wilayani kwa ajili ya kuchangia duka la dawa la wilaya. Aliongeza kwamba Bima ya afya ya jamii itabeba jumla ya watu sita katika kila kaya yaani mume, mke na watoto wanne. Aidha kwa familia ambazo zitakuwa na watu zaidi ya sita basi wale waliosalia wanaweza kuunganishwa na familia ya nyingine yenye watu zaidi ya sita na wakachanga elfu kumi na tano inayotakiwa na kupatiwa kadi ya pamoja kwa ajili ya matibabu. Aliwasihi wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii ili kunufaika nao. Aliwapa rai kuwa haimaanishi kwamba watatibiwa magonjwa yote bure au watapata matibabu ya aina yote bure. Kuna baadhi ya matibabu ambayo wananchi watapaswa kuchangia pesa kidogo. Baadhi ya vitu ambavyo watapaswa kuchangia ni pamoja na masuala yote ya upasuaji na utra sound.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa