- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amesema kaya masikini zipatazo 1,106,071 hapa nchini, zinanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini wa TASAF awamu ya tatu uliozinduliwa Agosti 15, 2012 mjini Dodoma.
Mkuu huyo wa wilaya Lt. Col. Michael Mntenjele, ameyasema hayo Aprili 09, 2018, wakati akizindua mafunzo ya siku tano ya wakufunzi, kuhusu kuunda vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza, kwa walengwa wa mpango huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
“Sisi tu mashahidi wa mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa TASAF katika awamu mbili zilizotangulia, ambapo TASAF awamu ya kwanza miradi 1,704 yenye thamani ya shilingi bilioni 72, ilitekelezwa na awamu ya tatu ilitekeleza miradi 12,347, yenye thamani ya shilingi bilioni 430.” Alisema Lt. Col. Michael Mntenjele.
Amewataka wanaonufaika na mpango huu kutumia vizuri fursa hii, kwani kuna wahitaji wengi, ambao wengependa kupata bahati hiyo, lakini hawakufanikiwa, kwani idadi ya kaya zilizotambuliwa ni 1,369,649, lakini zilizonufaika ni chache.
Aidha, amesema mpango huu unatekeleza miradi ya kutoa ajira za muda, na inatekelezwa katika Halmashauri 44, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ikiwa mojawapo.
Amewataka wanamafunzo hao kuwa makini na wasikivu, kwani mafunzo hayo yatawajengea uelewa, ili waweze kutekeleza shughuli za kuweka akiba na kukuza uchumi kwa kaya masikini kwa ufanisi mkubwa.
Mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku tano, yanawashirikisha wajumbe toka katika vijiji vya mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wajumbe toka mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa