- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wa Kijiji cha Kazingati kata ya Keza katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wameiomba serikali imruhusu mwekezaji toka nchini Korea Kusini awekeze kijijini humo, ili waweze kunufaika na ajira pamoja na tecknolojia ya kilimo cha kahawa na mpunga itakayokuja na mwekezaji huyo.
Wananchi hao wameyasema hayo wakati wakiongea na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Mh. Alex Gashaza (CCM) wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kazingati Januari 02, 2019 baada ya kuwepo malalamiko ya kwamba anapinga wawekezaji kupata ardhi kijijini humo.
Katika mkutano huo wananchi wamepinga hoja ya Mbunge kwamba, haukufuatwa utaratibu wa kugawa ardhi ya kijiji hicho kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini; “tuliitwa na Mwenyekiti wa kijiji, akatuuliza kuhusu kutoa ardhi yetu kwa mwekezaji wa Korea Kusini tulimkubalia tukitarajia kupata ajira.” Alisema Ndugu Daniel.
Wamesema kwamba wanaridhia wawekezaji wa taifa hilo, kuanzisha miradi ya maendeleo kijijini kwao, wajipatie ajira ili wajikwamue kiuchumi; huku wakidai ardhi iliyopo ni maeneo ya wazi hawanufaiki nayo ukiachilia mbali watu wasiowanakijiji kuyafanya malisho ya mifugo.
“Sisi wananchi wa kijii cha Kazingati tunamtaka mwekezaji toka Korea Kusini, ili tupate ajira na kunufaika na teknolojia mpya itakayokuja na mwekezaji huyo, kwani ardhi iliyopo katika kijiji hiki inatosha kuwekeza; wewe unapinga wawekezaji lini tutapata ajira na kufaidika?” Alihoji mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Ndugu Mathayo Daniel.
Ndugu Daniel amesema ardhi hiyo imejaa ng’ombe wanaotoka kwa wafugaji wa nje ya kijiji hicho, lakini wananchi wa kazingati hawanufaiki ispokuwa viongozi; huku akitaka wawekezaji hao waruhusiwe kuanzisha miradi yao katika ardhi hiyo.
Mbunge wa Ngara Mhe.Alex Gashaza anapinga kutolewa ardhi kwa wawekezaji wa Korea Kusini baada ya kusainiwa mkataba (MOU) wa kupewa ardhi ekari 12,000 wakati na wananchi wa Kazingati wameridhia.
Aidha madai ya Mbunge huyo ni kwamba hakuna kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara kilifanyika kupitisha kugawa ardhi ya kijiji cha Kazingati ambayo ilibainishwa kwenye vitongoji vya vya Muko na Msalasi vyenye ukubwa usiozidi ekari 4,140.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara,Mhe. Erick Nkilamachumu amesema, utaratibu wa kutoa ardhi ulifuatwa na malengo ni wananchi kupata miradi ili waweze kujiinua kiuchumi, na si vinginevyo.
Amesema matarajio ya Halmashauri ilikuwa kupata wawekezaji kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati wa viwanda, ambapo hata Wilaya ya Ngara ingesonga mbele kwani wawekezaji hao wangelipa mapato
"Mgogoro huo hadi Halmashauri iufikishe Wizara ya Ardhi kwa Waziri mwenye dhamana ndiye atakayeweza kuutolea ufafanuzi badala ya kujibia hoja mkanganyiko nisijichonganishe na wananchi ".Amesema Nkilamachumu
Mbunge huyo Gashaza amefanya mkutano huo January 2, 2019 ikiwa ni siku chache baada ya Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa kuagiza uongozi wa wilaya ya Ngara kuacha mara moja mipango ya kugawa ardhi kwa mwekezaji kutoka korea Kusini.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa