- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watendaji wa kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwafuatilia wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidoto cha kwanza kabla ya Machi 30, 2018, ambayo ni siku ya mwisho ya kwaandikisha wanafunzi hao.
Hayo ni kwa mujibu wa Kaimu Afisaelimu Idara ya Elimu Sekondari Ndugu Marton James akiwa ofisini kwake, kwamba hadi Machi 09, 2018 wanafunzi mia nne (400) walikuwa hawajaripoti shuleni.
“Wanafunzi wapatao elfu tatu mia nne kumi na wawili (3412), kati ya elfu tatu mia nane kumi na watatu (3813) waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, wameripoti shuleni katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.” Alifafanua Ndugu James.
Amewataka watendaji hao wa kata kuwafuatilia wazazi wa watoto wote, ambao hawajaripoti shuleni wahakikishe wameandikishwa shule, na atakayekiuka agizo hili itabidi sheria ichukue mkondo wake.
Aidha, amezitaja shule zilizofanya vizuri katika kuwaandikisha watoto hao kuwa ni; Rusumo iliyopokea watoto hao kwa 100%, Murugwanza kwa 98.40%, Kirusha kwa 97%, Bukiriro kwa 96.64%, pamoja na Mugoma iliyofikisha 96.43%.
Shule ambazo hazijafanya vizuri ni Murusagamba iliyoandikisha vijana kwa 81.29%, Muganza kwa 79%, Nyakisasa kwa 79.07% na Muyenzi iliyoandikisha wanafunzi 74.59% pekee.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa