- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara Leo
Kimefanyika kikao Cha kamati ya ushauri Wilaya ya Ngara (DCC) Katika ukumbi wa Community Centre uliopo Ngara Mjini.
Kikao hicho kimeongozwa na katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani Ally Lukali* Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Col Mathias J. kahabi ambapo Katibu wa kikao hicho akiwa Ndg. Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya pia kimehudhuliwa na Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara, Makamu Mkiti Halmashauri Mhe. Adronizi Bulindori, kamati ya Usalama Wilaya, Waheshimiwa Madiwani , Wakuu wa Idara na Vitengo Vya Halmashauri, Wakuu wa Taasisi za Serikali, na zisizo za Serikali, viongozi wa Madhehebu ya Dini , Maafisa Tarafa, watendaji wa kata.
Kikao hicho kimepitia Rasimu ya bajeti 2024/2025 na mapitio ya Bajeti 2023/2024. ambapo taarifa imewasilishwa na Mkuu Wa Idara ya Mipango na uratibu Wilaya Ndg Constantine Msemwa Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Mkiti wa kikao hicho Bi Hatujuani alitoa nafasi Kwa wajumbe kuchangia pia kutoa ushauri.
Aidha Maoni ya mapendekezo ya Bajeti Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kutoka Kwa wadau wa Halmashauri yamepokelewa Kwa Maboresho zaidi ya Bajeti hiyo.
Wakuu wa Idara za Elimu Msingi ,Sekondari na utawala ,utumishi na raslimali watu wakiwa kwenye Kikao Cha kamati ya ushauri Wilaya - DCC Kilichofanyika Ukumbi wa Community Centre Ngara mjini.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kikao.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Community Centre Ngara mjini.
Mhashamu Baba Askofu Jimbo la Rulenge Ngara Severine Niyomugizi aliyekaa akiwa kwenye Kikao Cha Kamati ya ushauri Wilaya kilichofanyika community center Ngara mjini.
Wajumbe wa Kamati ya usalama na viongozi wengine wakiwa kwenye Kikao.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao.
Makamu Mkiti Halmashauri ya Wilaya Adronizi Bulindori akiwa na Wakuu wa Idara ya kilimo na Mifugo Ndg Josephat Sangatati na Mkuu wa kitengo Cha ukaguzi wa Ndani Ndg T. Ngerangera.
Bi Hatujuani A Lukali katibu Tawala Wilaya( kulia) , Ndg Solomon O Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya( katikati) na Mhe Wilbard Bambara Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya( kushoto).
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa