- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe. Hatujuani Ally Lukali Katibu Tawala wilaya ya Ngara ambaye
Alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe. Col. Mathias Julius kahabi katika kikao Kilichofanyika tarehe 17/11/2023 ambapo ilisomwa taarifa ya Maendeleo ya Miradi ya Maji Wilaya ya Ngara.
Mhe Katibu Tawala Wilaya Aliwaomba wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji na kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuboresha miundombinu zaidi na kwamba hatua Kali zitachukuliwa kwa watakao haribu vyanzo vya maji .
Aliendelea Kwa kusema ambaye hatalipia huduma ya maji ikiwemo kukatiwa huduma hiyo.
Katibu Tawala wilaya aliwataka wakandarasi wote wanaofanya kazi na kupitiliza muda wa makubaliano (Wazembe) hawatovumiliwa na watachukuliwa hatua Kali zakisheria .
Katibu Tawala wilaya amewapongeza viongozi wa RUWASA-Ngara Kwa Juhudi wanazozifanya kuhakikisha huduma ya Maji safi inapatikana .
Nae Eng. Jumanne Magugu katika kikao hicho amewaasa wananchi kujitokeza kulipa huduma ya maji kwawakati ili kuboresha huduma zaidi na iwafikie wananchi ambao bado hawajapata huduma ya maji,
Eng huyo amewaomba wananchi kutunza vyanzo vya maji na kutoa taarfa za uharibifu wa makusudi wa vyanzo vya maji na kwamba Kila mmoja awe mlinzi wa vyanzo hivi kwa manufaa ya wananchi wote.
Eng Jumanne amewaomba viongozi wote kuanzia vitongoji, vijiji, kata na wilaya katika suala Zima la utunzaji wa vyanzo vya maji. Pia wajitahidi kukusanya mapato ili pesa hizo ziboreshe huduma za maji .
Mwisho Katibu Tawala wilaya aliipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maji ambayo inawanufaisha wana Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa