- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kimefanyika Kikao kilichoshirikisha Wafanyabiashara na wakulima wa Parachichi katika Ukumbi wa Community Centre Ngara Mjini.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa na katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani Ally Lukali akimwakilisha Mkuu wa wilaya Mhe Col. Mathias kahabi, pia kilihudhuriwa na M/kiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon O Kimilike, Mbunge Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba Ruhoro , Mhe Diwani Kabanga Wakuu wa Idara za kilimo, Biashara , Mwanasheria wa Halmashauri, Afisa ushirika Wilaya, Maafisa kilimo na Mtendaji Kata Kabanga.
Mkiti wa kikao Bi Hatujuani Ally Lukali alitoa nafasi Kwa wafanyabiasha pia wakulima baada ya hapo alitoa nafasi Kwa viongozi Mhe Mbunge Jimbo la Ngara, Mkiti wa Halmashauri.
Mwisho yalitolewa maazimio Kama ifuatavyo:
Ichukuliwe takwimu za Parachichi zinazotoka nje ya nchi na zinazopatikana ndani ya nchi (TPHPA,watendaji , Wataalam).
ufanyike ukaguzi wa Parachichi zinazoingia ndani ya Wilaya na uzuia kama hazina Ubora (TPHPA).
Ufuatiliwe mwenendo wa Bei na kuweka Mkakati wa soko la ndani.
Ufanyike ukaguzi wa mara Kwa mara Kwa wafanyabiasha wanaojaza Lumbesa. kila Mfanyabiashara atumie mizani kupima Parachichi.
Watambulishwe wanunuzi wote wa Parachichi waliopata vibali vya kununua Parachichi Kutoka Wizara ya kilimo Kwa wakulima.
Wafanyabiashara na Wakulima wa parachichi katika kikao hicho Kilichofanyika ukumbi wa community centre Ngara Mjini.
Viongozi wakiwa kwenye kikao Cha wafanyabiashara na Wakulima wa Parachichi.
Kikao Cha Wakulima wa Parachichi na Wafanyabiashara Kilichofanyika katika ukumbi wa community centre Ngara Mjini.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa