- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, vilivyokuwa vinatumika kabla ya mifuko haijaungana viendelee kutumika hadi mwaka 2023.
Rais Magufuli amesema hayo leo, alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika kujadili kikokotoo kipya cha mafao kwa wastaafu.
“Kustaafu sio dhambi, bali ni heshima na mtu anayestaafu ni shujaa; aliyetumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu kwa kutimiza majukumu yake, vivyo hivyo hatakiwi kubughudhiwa” Amesema Magufuli
Amesema kikokotoo hicho kitakuwa cha kipindi cha mpito ambapo kufikia mwaka 2023, jumla ya wasaafu 58,000, wataendelea kulipwa 50% ya mafao yao kwa mkupuo, badala ya kupokea mafao ya 40% yaliyopendekezwa hapo awali.
Amesema watumishi hao, kwa kigezo cha kupewa mafao yao kwa 25% ni kuwaongezea msongo wa mawazo na kushindwa kutekeleza malengo ya maisha yao; huku wakiendelea kuilalamikia serikali inayojali watu wanyonge.
Mifuko ya jamii inayojihusisha na kikokotoo cha wastaafu ina jumla ya wanachama 1,261,200 ambayo iliunganishwa katika mifuko miwili ya NSSF NA PSSSF; kabla ilipendekeza kutoa 25% kwa wastaafu kitendo kilichokuwa kinapelekea kuilalamikia serikali.
Aidha, amesema katika kuendelea kuwafahamu watumishi mamalaka ikiwemo mifuko ya jamii, wizara ya utumishi, kuhakikisha inafanya uchunguzi wa wastaafu hewa, lakini mifuko hiyo ijielekeze kwenye uanzishaji wa miradi yenye tija.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagiza wanasheria , watendaji wa serikali na vyombo vya dola, kufanya uhakiki wa orodha ya wastaafu kwani, wanaweza kuwepo wastaafu hewa, hivyo ameagiza zoezi la kuwahakikia wastaafu hao lianze mara moja.
Vile vile, amewataka wanasiasa kutoingilia mifuko ya hifadhi ya jamii, kwamba waiache ifanye kazi yake; huku akiwataka watumishi wa mifuko hiyo wasijihusishe na vitendo vya kupokea Rushwa kutoka kwa wastaafu ispokuwa wafanye kazi kwa kutenda haki na kufuata sheria.
“Hili litaondoa ubadhilifu na ukiukaji wa maadili ya utumishi, wastaafu wataweza kunufaika na mafao yao lakini pia itaondoa manung’uniko kwa baadhi ya kanuni au sheria zinazolalamikiwa na watumishi wastaafu” Ameongeza Rais
Rais Magufuli ameitaka mifuko hiyo, kujitathimini katika matumizi ya mali ya wafanyakazi hasa katika suala la utoaji wa ajira ya walinzi kutoka kwenye makampuni binafsi na kuwalipa zaidi ya Shilingi bilioni 4, ambapo kama mifuko hiyo ingewaajiri Suma JKT wangelipa shilling shilingi 1.4 bilioni pekee kwa mwaka.
“Mifuko ya hifadhi ya jamii ipunguze matumizi ya ovyo na kusifanyike uwekezaji usio na tija, lakini ipunguze gharama za uendeshaji na kuwaunganisha watumishi wa sekta binafsi wapatao 448,000 katika mifuko ya NSSF.” Aliongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli amehitimisha kwa kusema kwamba vikokotoo vinavyotumika kwa wasataafu vitofautiane na muda wa kila msataafa huku akisistiza kuwa, mifuko hiyo itafute wanachama zaidi kutoka hata sekta binafsi, na kulipwa mafao yao mara tu wanapomaliza mikataba yao.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa