- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
● Zoezi la ulipaji fidia wananchi lazinduliwa Wilayani Ngara,Kagera
● Kaya 1339 kulipwa fidia
● Wananchi 800 wameisha saini Mikataba ya Malipo
Imeelezwa kuwa takribani Kaya 1339 katika Wilaya ya Ngara wanatarajia kulipwa kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 26 ikiwa ni sehemu ya fidia ya ardhi iliyotolewa kupisha mradi wa uchimbaji wa Madini Mkakati ya Nikeli katika eneo la Bugarama Mkoani Kagera ambapo madini hayo ya Nikeli yatakayochimbwa yatachenjuliwa na kusafishwa hapa hapa nchini Tanzania kupitia kiwanda cha kisasa kitakachojengwa Kahama,Mkoani Shinyanga.
Hayo yameelezwa leo Novemba 14 , 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha eneo la Mradi wa Uchimbaji wa Madini Mkakati ya Nikeli iliyofanyika katika viwanja vya Mgodi wa Kabanga Nikeli Mkoani Kagera.
Waziri Mavunde ameeleza kuwa Mradi huu ni wa historia katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara ambao utatumia Teknolojia ya kisasa katika Uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini hayo nchini ambapo teknolojia itakayotumika ni ya kisasa ya hydro met.
Akielezea kuhusu Mipango ya Serikali katika uchimbaji wa Madini Mkakati , Waziri Mavunde amebainisha kuwa kwasasa Serikali inaandaa mkakati wa usimamizi wa madini ya kimkakati na hasa katika kusimamia uongezewaji thamani wa madini hayo hapa hapa nchini.
Sambamba na hapo Waziri Mavunde amesisitiza kuwa Serikali inachukua Mradi wa Tembo Nikeli kama sehemu ya Mradi wa kielelezo kwa Miradi mingine ya Madini Mkakati inayofuata.
Akitoa maelezo yake Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema kwamba serikali inatambua umuhimu wa mradi huu mkubwa wa kielezo na kwamba wizara ya ardhi itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kwamba zoezi la fidia linakamilika kwa wakati na wananchi wanapata haki yao kwa mujibu wa Sheria.
Wakitoa maelekezo ya Kamati za Bunge za Ardhi,Maliasili na Utalii na Nishati na Madini,Waheshimiwa Timothy Mnzava na Kirumbe Ng’enda wameitaka Kampuni ya Tembo Nikeli kuhakikisha inalipa fidia kwa wakati kwa wananchi wanaopisha mradi huo wa kimkakati.
Zoezi la uzinduzi wa ulipaji fidia lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa, Wajumbe wa Kamati za kuduma za Bunge zinazosimamia sekta za Ardhi na Madini,pamoja na Mbunge wa Ngara Mhe. Ndaisaba G.Ruhoro na wa viti maalum Mhe. Oliva Semguruka.
Aidha viongozi wengine walioshuhudia ni Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias Kahabi, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike, kamati ya Usalama ,Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri pia viongozi Mbalimbali wa chama na serikali.
Zoezi la ulipaji fidia wananchi Waguswa wa Mradi wa Tembo nickel wazinduliwa wilayani Ngara Kagera
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa