- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo limefanyika kongamano la miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara pamoja na zoezi la Uchangiaji Damu .
Kongamano na zoezi la Uchangiaji Damu Yamefanyika katika ukumbi wa community center Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara Mjini .
Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara KI-WILAYA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi.
Waliohudhuria kongamano la Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara katibu wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ngara, Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya,Mbunge, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya,kamati ya Usalama, viongozi wa madhehebu ya dini, Wakuu wa Idara na Vitengo, Taasisi/Mashirika ya Serikali na Binafsi, wazee maarufu, chuo Cha Maendeleo ya wananchi Lemela, Skaut, watumishi Mbalimbali wa makao Makuu, wakulima, wafugaji , wafanyabiashara , wanahabari, na Wananchi.
Kauli mbiu ya Maadhimisho "UMOJA NA MSHIKAMANO NI CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
Kaimu katibu Tawala wilaya amesoma taarifa fupi ya wiki ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru Wa Tanzania Bara wilayani Ngara Mkoa wa kagera.
Ambapo shughuli zilizofanyika ni kupamba Ofisi za Serikali Kwa bendera ya taifa, kuwepo Kwa vitabu vya kusaini, uhamasishaji juu ya Maadhimisho kupitia vyombo Mbalimbali vya Habari, kuongea na wazee maarufu/ watumishi wastaafu,kufanyika zoezi kabambe la Usafi na upandaji miti jumla ya miti 7008 imepandwa kata 22 ,kufanyika Kwa matembezi ya kilometa 5, kufanyika Kwa mazoezi ya pamoja AEROBIC, kufanyika Kwa michezo ,kufanyika kongamano / Mdahalo na zoezi ya uchangiaji damu salama.
Aidha zimetolewa shukrani Kwa wadau Mbalimbali wamechangia vitu Ambao ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya , Ngara oil, Nmb, Galaxy club( kolonery),Ngara famers,Chama Cha walimu,RUWASA,na CARITAS Rulenge.
Katibu wa chama Cha Mapinduzi Bi Anastazia Amas alisema Tanzania tumepiga hatua kubwa tofauti kubwa wakati tunapata uhuru aidha Alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa anayoifanya awamu ya sita.
Mwakilishi wa Mbunge na Mkiti wa Halmashauri ambaye ni Diwani Mhe Kennedy staford aliipongeza serikali Kwa hatua kubwa ambayo imefanya ya kuwaletea Maendeleo wananchi huku akitoa mifano Mbalimbali ya Sekta ya Afya ,Elimu, maji na Barabara Kwa Wilaya ya Ngara.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuleta Fedha nyingi Kwa ajili ya miradi ya Maendeleo Kwa wananchi Sekta za Elimu,Afya, maji , Barabara nk.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ngara aliendesha Mdahalo/ kongamano huku akitoa tofauti Mbalimbali zilizopo kabla ya uhuru, wakati tunapata uhuru na baada ya uhuru. Aidha Alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwaletea Miradi ya Maendeleo Kwa wananchi , maji, vyumba vya Madarasa Shule za Msingi na Sekondari,umeme , Barabara na vituo vya afya / Hospitali.
Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi aliye katikati Mgeni Rasmi katika maadhimishoyl ya miaka 62 ya uhuru akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike ,katibu wa Ccm Wilaya Bi Anastazia Amas, kaimu katibu Tawala Ndg Jawadu Yusuph pamoja na viongozi wa madhehebu ya Dini.
Wadau Mbalimbali wakiwa kwenye kongamalo la miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara katika ukumbi wa Community center Ngara Mjini.
Viongozi Mbalimbali na wanachi wakiwa kwenye kongamano la miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara wilayani Ngara.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathis J.kahabi akiwa na Afisa utumishi, Mkurugenzi Mtendaji, katibu wa chama Cha Mapinduzi , kaimu katibu Tawala na Wakuu wa Idara Halmashauri.baada ya Kumaliza kongamano ukumbi wa community center.
Kongamano la miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara wilayani Ngara. Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias Kahabi.
Kongamano la miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara.
Mkuu wa Wilaya Ngara Mhe Kanali Mathias J Kahabi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike kwenye Kongamano la miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara ukumbi wa community center.
Mhe Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi akiwa na kamati ndogo ya uratibu wa wiki ya Maadhimisho.
Zoezi la Uchangiaji Damu limefanyika eneo lililofanyika kongamano la miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa